Kupitia ukurasa wa mtandao mmoja maarufu wa kijamii nchini,
mwigizaji wa vichekesho na filamu nchini, Kitale almaarufu kama Mkude
Simba amemwamgia sifa kedekede mwigizaji mwigine anayefanya vizuri
kwenye upande wa filamu nchini Riyama Ali kama ishara ya kuonesha upendo
wake kwa mwanadada huyo.
Huku akiwa ameweka picha ya mwanadada Riyama, Kitale aliandika:
"Huyu mdada mm napenda kumuita kambi popote kwa
maana ya kwamba achagui scene yy ukimpa scene yoyote ile kwake twende
anacheza, ongera kwa hilo kwanza kwa sababu hiyo ndio sifa kubwa ya
msanii kiukweli anajua anastahili sifa maana mpaka anakera mh! cjui
niseme anaboa..!! ww mdada unajua mpka unaboaaaa"
Comments
Post a Comment