Posts

Showing posts with the label SIASA NA UCHUMI

Mkuu wa Wilaya Lucy Mayenga Aihofia Kasi ya Magufuli..Ajisalimisha na Kumuomba Rais Asimchague Tena Ukuu wa Wiliya

Image
Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote. Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti. Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zin...

Mheshimiwa Zitto Kabwe Amuomba Rais Magufuli Atengue Agizo la Jakaya Kikwete

Image
Mheshimiwa Zitto Kabwe Amuomba Rais Magufuli Atengue Agizo la Jakaya Kikwete Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anatafuta nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli kumuomba atengue agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzuia ujenzi wa makazi katika Mlima wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji. Rais Kikwete alitoa agizo hilo mwaka 2006 kama moja ya hatua za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na kujaa mchanga kwa bandari ya Kigoma. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kigoma Cinema mjini Kigoma, Mbunge huyo alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuamini kwamba taarifa alizopewa Rais Kikwete zilizosababisha kutoa agizo hilo hazikuwa sahihi. Zitto alisema Rais Kikwete alipewa taarifa potofu kwamba mmomonyoko wa udongo kutoka katika eneo hilo ndiyo unaosababisha kujaza mchanga na kupunguza kina katika bandari ya Kigoma. Mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema kuwa tafiti zilizofanyika na taarifa zilizopo zinaonesha kuwa kup...

Waziri Mkuu Kuanza kutembelea miradi ya serekali ambayo inatakiwa kuwa nufaisha wananchi wa kanda ya ziwa.

Image
Waziri Mkuu Kuanza kutembelea miradi ya serekali ambayo inatakiwa kuwa nufaisha wananchi wa kanda ya ziwa. juliusjoseph.blogsport.com Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa leo anatarajia kuanza ziara ya siku 14 katika mikoa ya Kanda Ziwa kukagua shughuli na miradi ya maendeleo.

CHADEMA : KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) KITAFANYA KIKAO CHAKE KESHO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
CHADEMA : KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) KITAFANYA KIKAO CHAKE KESHO JIJINI DAR ES SALAAM Posted by Julius Joseph On Thursday, January 02, 2014 No comments  John Mnyika-Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema --     CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho,Chama kimetoa kauli ifuatayo; Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu; Mosi:  Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katib...

JAJI WARIOBA: KATIBA YA TANGANYIKA INAWEZA KUPATIKANA KWA MIEZI MITATU.

Image
JAJI WARIOBA: KATIBA YA TANGANYIKA INAWEZA KUPATIKANA KWA MIEZI MITATU. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mkutano wake na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Dar es Salaam jana.  Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Katiba ya Tanganyika inaweza kuandikwa ndani ya miezi mitatu tu kwa kuwa maoni mengi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyozinduliwa Jumatatu, kwa kiwango kikubwa yametoka kwa wananchi wa upande huo wa Muungano Warioba alisema hayo jana wakati akizungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. “Kutunga Katiba ya Tanganyika siyo kazi ngumu, ukisoma rasimu hii sura ya kwanza mpaka ya tano, sioni kama Katiba ya Tanganyika itakuwa tofauti na maoni yaliyomo katika sura hizo,” alisema na kuongeza: ...

CCM; PINDA NA HAWA GHASIA WANG'OKE

Image
CCM; PINDA NA HAWA GHASIA WANG'OKE   Rais Jakaya Kikwete, ameshauriwa kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikielezwa sababu kuwa ndiye kikwazo katika utendaji wa Serikali na kwamba akiachwa ataipeleka pabaya Serikali na CCM. Kikwete pia ameshauriwa kumfukuza kazi Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, kwa kushindwa kukabiliana na matatizo ya ubadhirifu katika halmashauri nchini. “Kama (Rais) unaitakia mema nchi na CCM kuchukua hatua za kuwafukuza kazi Pinda na Waziri Ghasia,” alisema Mbunge wa Mwibara, Khangi Lugola (CCM), juzi alipochangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka jana. “Kwa nini Watanzania wafe kwa kunyimwa misaada na wafadhili kwa sababu ya mtu mmoja tu Pinda, kwa ajili ya Ghasia ameiendesha Tamisemi kama Saccos ama Vikoba?” alihoji.  “Mchawi wetu ... ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekuwa mpole mno hawajibiki,” alisema Mh. Lugola na kuongeza, “Kuanzia j...

Taswira:Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa Aunguruma Kibondo na Kigoma aliyekuwa Mwenyekiti Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM, Sevelino Damian ajiunga na Chadema

Image
Taswira:Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa Aunguruma Kibondo na Kigoma aliyekuwa Mwenyekiti Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM, Sevelino Damian ajiunga na Chadema Written by haki | // 0 comments   Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Community Center mjini Kibondo   Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akipokea kadi ya uanachama, kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM, Sevelino Damian, ambaye amehemia Chadema, wakati wa mktano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwa kushirikiana na wananchi, wakimdhibiti mmoja wa vijana waliofanya fujo katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika katika kijiji cha ...

AFRIKA MASHARIKI:MARAIS WA KISAINI MAKARATASI YA KUTUMIA SARAFU MOJA.http://juliusjosephsp.blogspot.com/

Image
MAKARATASI YA KUKUBALI KUTUMIA SARAFU MOJA Posted by Gadiola Emanuel On Saturday, November 30, 2013 No comments Today we signed the Monetary Union Protocol which will provide for a wide scope of co-operation in monetary and financial sectors among the EAC Partner States and will further catalyze trade growth within the region. We are now a people destined for greatness, prosperity and happiness. Our borders are fast becoming mere formalities. As we integrate, we cease to be a group of neighbouring nations, and become one people. Let us think with one mind, speak with one voice and walk on one road to our promised destination, “A better East Africa for all its citizens”. H MAKARATASI YA KUKUBALI KUTUMIA SARAFU MOJA Posted by Gadiola Emanuel On Saturday, November 30, 2013 No comments Today we signed the Monetary Union Protocol which will provide for a wide scope of co-operation in monetary and financial sectors among the EAC Partner Sta...