TCME WASHIRIKIANA NA VETA KATIKA KUTOA MAFUNZO
TCME WASHIRIKIANA NA VETA KATIKA KUTOA MAFUNZO Mgeni Rasmi katika sherehe za mwaka za Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizugumza kwa niaba ya Waziri kwa wageni waalikwa na mabalozi.(Picha na Zainul Mzige) . Joseph Kahama aahidi ushirikiano na wachimbaji wadogo nchini .Asema sekta ya madini kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa Na Damas Makangale, MOblog Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Joseph Kahama amesema chama kwa kushirikiana na chuo cha Ufundi Veta Moshi wataendelea kupeleka vijana wazawa wa kitanzania kwenda kupata mafunzo ya mambo ya uchimbaji na utafutaji wa Madini (Geology). Akizungumza na MOblog jana kwenye mahojiano maalum baada ya kumaliza mkutano wao wa mwaka kwa wanachama wake, Joseph Kahama amesema chama chao kwa kushirikiana na serikali wataendelea kusaidia vijana ...