Posts

Showing posts with the label HABARI ZA KITAIFA

Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA.

Image
Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA. Siku ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa  wanawake.   Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945,ilipofika tarehe 8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee.   Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali z...

Jamii Forums Wakimbilia Mahakamani....Wadai Kushinikizwa na Jeshi la Polisi Kutoa Siri za Wachangiaji wao

Image
Jamii Forums Wakimbilia Mahakamani....Wadai Kushinikizwa na Jeshi la Polisi Kutoa Siri za Wachangiaji wao Kampuni ya Jamii Media ambayo ni wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya Jamii Forums na FikraPevu, wamefungua kesi ya Katiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga amri waliyopewa na polisi ya kutoa taarifa binafsi za wanachama wao. Akizungumza baada ya kufungua kesi hiyo jana, Wakili wa Jamii Media, Shukuru Mkwafu alisema lengo lao ni kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwani vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Wakili Mkwafu alisema ili kulinda masilahi ya umma, lazima vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vizingatiwe. Alisema Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka 2015, inakiuka haki ya kikatiba namba 16 inayoruhusu kuwapo na hali ya faragha na kifungu namba 18 kinazungumzia uhuru wa kujieleza. Mmiliki wa tovuti...

Rais Magufuli Ampongeza Francis Cheka kwa Kutwaa ubingwa wa Mabara wa Uzito wa Super-Middle

Image
Rais Magufuli Ampongeza Francis Cheka kwa Kutwaa ubingwa wa Mabara wa Uzito wa Super-Middle Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amempongeza bondia Francis “SMG” Cheka kwa kutwaa ubingwa wa Mabara wa uzito wa Super-Middle wa chama cha WBF baada ya kumtwanga kwa pointi bondia Mserbia, Geard Ajetovic. Cheka alimchapa Ajetovic kwa ushindi wa majaji wote wa tatu katika pambano gumu lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club. Akitoa pongezi hizo jana, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa Rais amefuraishwa sana na ushindi wa Cheka ambao umeipa heshima nchi katika medani ya michezo ndani na nje ya mipaka yake.

Maalim Seif Arejea Zanzibar Akitokea India Kwenye Matibabu......Mamia ya Wafuasi wake Wampokea, Asema Polisi Imegeuka tawi la CCM

Image
Maalim Seif Arejea Zanzibar Akitokea India Kwenye Matibabu......Mamia ya Wafuasi wake Wampokea, Asema Polisi Imegeuka tawi la CCM Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana aliwasili Zanzibar kutoka ughaibuni na kulilaumu Jeshi la Polisi nchini akisema, “hapana shaka yoyote sasa limegeuka tawi la CCM.” Maalim Seif alisema hayo jana jioni wakati akizungumza na wafuasi wake waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume na baadaye kumsindikiza hadi nyumbani kwake Mbweni mjini hapa. Baadhi ya viongozi wa CUF waliohudhuria mapokezi hayo ni pamoja na Mansour Yussuf Himid, Nassor Ahmed Mazrui, Fatma Abdulhabibi Ferej na aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema chini ya mwavuliwa wa Ukawa katika urais wa Muungano, Juma Duni Haji. Maalim Seif aliyetokea India kupitia Falme za Kiarabu, alisema anaunga mkono kauli za Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wake, zilizosababisha ahojiwe na polisi juzi, kuwa “sasa CUF wamechoka na uhuni dhid...

Mkuu Wa Majeshi Aongoza Kuwaaga Maofisa Majenerali 16 Wa Jwtz Waliostaafu

Image
Mkuu Wa Majeshi Aongoza Kuwaaga Maofisa Majenerali 16 Wa Jwtz Waliostaafu MKUU wa Majeshi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange amewaongoza wanajeshi mbalimbali kuwaaga Majenerali 16 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambao wamemaliza muda wa utumishi wao. Sherehe hizo zilifanyika Uwanja wa Kambi ya Jeshi wa Twalipo, Mgulani jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana. Sherehe hizo ziliongozwa na bendi ya jeshi na gwaride maalumu. Miongoni mwa waliomaliza muda wao ni Meja Jenerali Samuel Ndomba ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na hadi anastaafu alikuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ. Wengine ni Luteni Jenerali Paul Mella ambaye alikuwa Kamanda wa Majeshi ya Kulinda Amani ya Darfur, Sudan na Brigedia Jenerali Harold Mziray ambaye alikuwa Mkuu wa Shule ya Infantria, Arusha. Majenerali wengine walioagwa ni Brigedia Jenerali Martin Mwankanye al...

Dkt. Bilal afungua kongamano la Kimataifa la Sayansi kwa nchi za Afrika na Kusini mwa jangwa la Sahara, Jijini Arusha

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa  Chuo cha Nelson Mandela cha jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. (Picha na OMR). Kongamano hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha  Agosti 5, 2014, na kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee na akina mama. Katika Hot...

HAPA NDIPO MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIPOTUNUKIWA SHAHADA LOONGTIME AGO........!!

Image
HAPA NDIPO MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIPOTUNUKIWA SHAHADA LOONGTIME AGO........!! Mwalimu akitunukiwa Shahada na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzee Msekwa. FROM LEFT:-

BREAKING NEWS: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LATAJWA HIVI SASA

Image
BREAKING NEWS: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LATAJWA HIVI SASA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LINATAJWA HIVI SASA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA NA KATIBU MKUU KIONGOZI,BALOZI OMBENI SEFUE.   - Hakuna Mabadiliko Ofisi ya Rais - Ofisi ya Makamu Wa Rais - Naibu Waziri Kitwanga amehamishwa na nafasi yake imejazwa na Mhe. Ali Mwalimu - Mwigulu Nchemba amekuwa Naibu Wizara ya Fedha (Sera). Aliyekuwa nafasi hiyo sasa ni Waziri Kamili - Uchumi na Mapato sasa anatoka Janet Mbene na inajazwa na Adam Malima - Asharose Migiro sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria - Ulinzi na Kujenga Taifa => Hussein Mwinyi - Mambo ya Ndani - Mathias Chikawe - Afya na Ustawi wa Jamii - Naibu wake sasa ni Waziri Kamili; naibu wa sasa ni Dr. Kebwe S. Kebwe - Mulugo ameondoshwa rasmi serikalini. Nafasi yake imejazwa na Jenista Muhagama - Pindi chana amejaza nafasi ya Ummi Mwalimu - Jinsia na watoto - Mifugo na Maendeleo ya Mifugo - Titus Kamani atakuwa Waziri mpya. Naibu ni Telele na hivyo Wizara nz...

MTANGAZAJI WA BBC IN FOCUS ON AFRICA `KOMLA DUMOR AFARIKI DUNIA

Image
R.I.P KOMLA DUMOR : MTANGAZAJI NGULI WA BBC 'FOCUS ON AFRICA' KOMLA DUMOR AFARIKI DUNIA Mwandishi wa BBC Komla Dumor amefariki ghafla nyumbani kwake kutokana na mshtuko wa moyo. Alikuwa na miaka 41 alipopata mauti yake.Komla Dumor ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika. Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemtaja marehemu kama zawadi ya Ghana ulimwenguni na kuongezea kuwa Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe wake. Komla hivi karibuni alikuwa anaongoza kipindi cha Runinga kinachozungumzia maswala ya Afrika baada ya kufanya kazi katika radio mmoja nchini Ghana na vilevile radio ya BBC. Mhariri wa habari za ulimwengu Andrew Whitehead amemtaja kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji. BBC SWAHILI

KIMATAIFA :TANZANIA JOINS FORCES WITH BRITAIN'S NO. 1 SCHOOL TO UNEARTH FOOTBALL TALENT.

Image
KIMATAIFA :TANZANIA JOINS FORCES WITH BRITAIN'S NO. 1 SCHOOL TO UNEARTH FOOTBALL TALENT. Eton Coach, Glen Pierce speaking at the press conference on Friday 10 Jan 2014 at Tanzania House London.  By Jestina George, “Tanzania has taken the first step towards producing their first Premier League player – thanks to Eton College, England’s premier public school. Together with Safarihub and charity organisation ACE Africa, Eton are sending Glen Pierce, head of sports, plus Ali Lyon, 19, Nicholas Zafirios, 18,  and Tom Pearson,18, who are on a gap year before starting university, to Tanzania to teach local children the finer arts of football. Ali has already passed his  Level 1 Football Association coaching badge and the quartet cannot wait for the challenge ahead of them. Coach Glen Pierce with Eton students who will be travelling to Tanzania, Nicolas Zafiriou, Ali Lyon and Tom Pearson Pierce said: “We are about to embark on a...