Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA.
Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA. Siku ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa wanawake. Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945,ilipofika tarehe 8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee. Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali z...