Posts

Showing posts with the label MICHEZO

Maneno ya kwanza ya Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle

Image
Jioni hii kwa hapa Tanzania habari zilianza kutoka kwamba Rafael Benitez amewasili St James Park kwa ajili ya kumalizia mambo ya mwisho mwisho. Guus Hiddink alisema kwamba Rafa Benitez ataleta uzoefu wa mkubwa kwa club ya Newcastle kama akiwa manager mpya wa club hiyo. Hatimaye Benitez amekua kocha mpya wa Newcastle united baada ya McClaren kufukuzwa kazi baada ya kikosi chake kuipeleka timu kwenye bonde la kushuka daraja. Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle alisema, “Nina furaha kuthibitisha kwamba nimefanya maamuzi na club kubwa ya England ambayo ina changamoto kubwa kwa sehemu ya ligi iliyobaki. Haitakua changamoto kubwa kwangu bali itakua kwa kwa wachezaji wangu,viongozi na mashabiki pia. Wote inabidi tuwe na lengo moja kwenye vichwa vyetu na nitaomba ushirikiano wenu kwenye hili.Mimi binafsi kurudi kwenye EPL ni kama kurudi kwenye familia yangu. Nahitaji ushiriki wenu kwa kikamilifu.”

Rais Magufuli Ampongeza Francis Cheka kwa Kutwaa ubingwa wa Mabara wa Uzito wa Super-Middle

Image
Rais Magufuli Ampongeza Francis Cheka kwa Kutwaa ubingwa wa Mabara wa Uzito wa Super-Middle Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amempongeza bondia Francis “SMG” Cheka kwa kutwaa ubingwa wa Mabara wa uzito wa Super-Middle wa chama cha WBF baada ya kumtwanga kwa pointi bondia Mserbia, Geard Ajetovic. Cheka alimchapa Ajetovic kwa ushindi wa majaji wote wa tatu katika pambano gumu lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club. Akitoa pongezi hizo jana, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa Rais amefuraishwa sana na ushindi wa Cheka ambao umeipa heshima nchi katika medani ya michezo ndani na nje ya mipaka yake.

Balaa Jipya Makalio ya Kichina na madhara yake

Image
Balaa Jipya Makalio ya Kichina na madhara yake Stori: Hamida Hassan na Boniface Ngumije D ar es Salaam: Tabia ya baadhi ya wasichana hasa wa mjini kuwa na tamaa ya kuwa na makalio makubwa na hivyo kulazimika kutumia dawa mbalimbali, imekuwa ikishamiri kila siku licha ya serikali kupiga marufuku uingizwaji wa dawa hizo. Jayjay Gazeti hili matoleo yaliyopita liliwahi kuandika jinsi mastaa wengi Bongo wanavyotumia dawa hizo lakini uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, kasi ya matumizi ya dawa hizo yamekuwa yakishamiri huku waathirika wengi wakijiuguza kwa siri baada ya kupata madhara. Gilla . Katika tukio jipya la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hamisa ambaye alidai ni mke wa mtu alisema kuwa, alishawishiwa na rafiki yake kutumia dawa hizo ili naye awe na ‘zigo’ lakini ameanza kuona zinamletea matatizo. “Nimekuwa nikisikia kuwa dawa hizi zina madhara lakini kuna rafiki yangu mmoja ambaye aliwahi kutumia na yuko poa...

Simba kushuka kijeshi, Kaseja azua hofu Mbeya City

Image
Simba kushuka kijeshi, Kaseja azua hofu Mbeya City Wachezaji wa Simba wakifanya yao. Nicodemus Jonas, Dar es Salaam BAADA ya kuwa mafichoni kwa takriban wiki moja mkoani Morogoro, kikosi cha Simba sasa kipo fiti, tayari kuwavaa Mbeya City katika mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Simba wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya lakini Simba ilikuwa chini ya Muingereza, Dylan Kerr wakati kwa sasa ipo chini ya Mganda, Jackson Mayanja. Meneja wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amewahakikishia Wanasimba kuwa kwa mazoezi waliyofanya, wana uhakika wa ushindi. “Kikosi kipo vizuri, bahati nzuri wachezaji karibia wote wapo, isipokuwa Hija Ugando ambaye alibaki Dar akiuguza majeraha, lakini wengine wote wapo kambini katika maandalizi ya mchezo huo,” alisema Gazza. Kipa wa Mbeya City, Juma Kaseja. Aidha, upande wa M...

Kiiza aandikiwa barua ya onyo kali Simba

Image
Kiiza aandikiwa barua ya onyo kali Simba Mshambuliaji wa Simba, Kiiza. Wilbert Molandi na Hans Mloli KATIKA kuhakikisha wanatengeneza nidhamu kwenye timu, uongozi wa Simba umeliagiza Benchi la Ufundi la timu hiyo kumuandikia barua ya onyo kali mshambuliaji wake Mganda, Hamis Kiiza. Hatua hiyo imekuja siku chache tangu uongozi wa Simba utangaze kumsimamisha beki na nahodha wake msaidizi, Hassani Isihaka kwa kile kilichodaiwa kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kocha wao Mganda, Jackson Mayanja. Mara ilivyotangazwa kusimamishwa kwa Isihaka, Kiiza alimtetea beki wake huyo katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kiliwakasirisha viongozi wa Simba. Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa tayari wamemuagiza meneja wa timu hiyo, Abbas Ally kumuandikia barua ya onyo mshambuliaji huyo. Taarifa kutoka ndani ya kambi ya Simba iliyopo Morogoro imeeleza kuwa Kiiza aliomba radhi kwa al...

Je Van Gaal ataumaliza msimu vizuri? Aiongoza United kushinda mechi ya 4 mfululizo

Image
Je Van Gaal ataumaliza msimu vizuri? Aiongoza United kushinda mechi ya 4 mfululizo  By Aidan Charlie - March 3, 2016 SHARE Facebook Twitter Mapema wiki iliyopita hakuna shabiki wa ambaye alikuwa anaamini timu yake ingeweza kupata matokeo chanya katika mechi 4 zilikuwa zinafuatana mfululizo za michuano tofauti, kutokana kiwango cha timu yao na udhaifu wa kikosi hicho kilichojaa majeruhi. Lakini chini ya kocha ambaye anaripotiwa kwamba siku zake za kuendelea kuwa mkufunzi mkuu wa timu hiyo zinahesabika – Manchester United imefanikiwa kushinda mechi zote zilizokuwa mbele yao. Baada ya kufungwa 2-1 na FC Mityjlland wiki mbili zilizopita, United waliifungua wiki iliyopita na ushindi wa 3-0 dhidi ya Shrewbury FC katika mchezo wa raundi ya 5 ya kombe la FA. Alhamisi ya wiki iliyopita Van Gaal na vijana wake wakawa na m...

Juve yaponea tundu la Sindano kwa Inter – Penati zawabeba. Fainali sasa vs AC Milan

Image
Juve yaponea tundu la Sindano kwa Inter – Penati zawabeba. Fainali sasa vs AC Milan By Aidan Charlie - March 3, 2016 SHARE Facebook Twitter Aibu nusra iwakumbe wakubwa usiku wa kuamkia leo huko Italia ndani ya Jiji la Milan. Mabingwa watetezi wa kombe la Coppa Italia Juventus leo wameepuka kuvuliwa ubingwa wao huo baada ya kukubali ushindi wao wa 3-0 katika mechi ya kwanza kule Turin kupinduliwa na vijana wa Roberto Mancini kwa kupigwa 3-0 na Milan ndani ya dakika 90 za mchezo marejeano. Lakini mwishowe bahati ikawa upande kwa kushinda kwa penati 5-3 na kutinga fainali.  Inter wakiingia kwenye mchezo huo wa nusu fainali ya pili ya Coppa Italia wakiwa na deni la magoli matatu waliyofungaa Turin January 27, walifanikiwa kupambana na kurudisha deni hilo kwa magoli ya Marcelo Brozovic dakika 16, Ivan Perisc akapiga l...

WACHEZAJI WALIOBEBA NDOO YA EPL BAADA YA KUONDOKA ARSENAL HATIMAYE KUIPA USHINDI MNONO TIMU YA MAN CITY UBINGWA

Image
WACHEZAJI WALIOBEBA NDOO YA EPL BAADA YA KUONDOKA ARSENAL Ni miaka 12 sasa Arsenal wanaweza kuadhimisha toka washinde kombe la Ligi kuu nchini Uingereza kwa mara ya mwisho, ni kitu kinachowauma sana sio mashabiki tu wa klabu hiyo lakini hata wachezaji pia. Ndiyo, mtu anaweza kusema kuwa Vijana wa Arsene Wenger ni wapinzani sahihi wa kombe wa kombe la Ligi kuu Uingereza msimu huu kutokana ana wapinzani wake wa muda mrefu Chelsea na Manchester United wote wakiwa nje ya Top Four. The Gunners kwa sasa wameachwa pointi sita wakiwa katika nafasi ya tatu na vinara wa ligi hiyo Leicester City, labda tusubiri na tuone kama vijana hao wa kasikazini mwa Jiji la London wataweka tabasamu katika nyuso zao kwa kuchukua kombe la Ligi kuu Uingereza ifikapo mwezi wa tano mwaka huu. Kuna baadhi ya wachezaji waliojaribu kusubiri kama Arsene Wenger,wakaamua kutimka Arsenal na kujiunga na vilabu vingine vya Ligi kuu Uingereza na wakafanikiwa kuchukua Kombe la Ligi k...

SERIKALI YATOA MOTISHA KWA WACHEZAJI WA TWIGA STARS

Image
SERIKALI YATOA MOTISHA KWA WACHEZAJI WA TWIGA STARS Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake(Twiga Stars) ikishinda katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa tarehe 4 machi katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam. Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia James Wambula alipotembelea kambi ya Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam. Akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao. Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi yake dhidi ya Zimbabwe kila m...

KOCHA Van Gaal tayari kupiga msasa Man U

Image
Man U imevutiwa na ukufunzi makini wa Van Gaal, lakini je ataweza kuirudisha M U kileleni? Huku ushabiki na mbwembwe za kombe la dunia zikibaki kumbukumbu,ushabiki sasa unarudi vilabuni, wana- Manchester United, wanamwangalia kwa karibu kocha wao mpya Louis van Gaal, amekuja na miujiza gani? Alipowasili kwenye uwanja wa mazoezi Carrington amesema hana jipya zaidi ya kujenga mshikamano zaidi miongoni mwa wachezaji. 'Ni lazima tuimbe wimbo huohuo ulioisaida timu ya Uholanzi ililowaezesha kukaribia ushindi wa kombe la dunia na kuibuka nafasi ya tatu kwa kuwafunga wenyeji Brazil' amesiitiza Lakini ufafanuzi zaidi ataotoa katika mkutano na waandishi habari baadae leo. Kikosi hicho cha Man United kikiwa na wachezaji wapya akina Herrera na Luke Shaw, waliopatikana kwa gharama ya zaidi ya £millioni 56m,wataelekea Marekani ijumaa kwa ziara na kucheza angalau mechi tano. ...

HATIMAYE MTANDAO WA MAWASILIANO TANZANIA VODACOM YACHANGIA MWENGE WA UHURU

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiongea ofisini kwake mjini Bukoba wakati wa hafla fupi ya kupokea mchango wa Sh. 10 Milioni kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya kuchangia sherehe ya uwashaji mwenge wa Uhuru kitaifa iliyofanyika Mkoani humo. Kutoka kushoto Ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Domician Mkama, Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni hioyo Salum Mwalim.  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akihakiki thamani ya hundi ya mfano iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom kuchangia sherehe ya uwashaji mwenge wa Uhuru kitaifa iliyofanyika Mkoani humo.Wanaofurahia kitendo hicho kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Domician Makama, Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Katibu Tawala wa Mkoa Nassor Mnambila (wa kwanza kulia). Makabidhiano hayo yalifanyi...

SHOW YA MSANI MAHIRI BONGO FLOVER YAINGIA DOA KWA MVUA ZINAZONYESHA JIJINI DAR

Image
  Lady jay Dee akiwa jukwaani. Mashabiki wakifuatilia shoo hiyo.… Lady jay Dee akiwa jukwaani. Mashabiki wakifuatilia shoo hiyo.   R Roma mkatoliki na Baghdaddy wakifanya makamuzi. Profesa Ludigo (Kulia) akiwa na Nikki Mbishi. Gadner akiwa na Profesa Jay. Wasanii wa Bongo Movie wakishauriana jambo. Patricia Hillary akiwa jukwaani kutoa shoo. Shabiki akimtuza Profesa Jay. Roma Mkatoliki akifanya makamuzi. Kutoka kushoto, Nando, Gadner na Profesa Jay. Mkoloni na Dokta Levy wakicheza. Vimwana wakipagawa na shoo. Profesa Jay akifanya makamuzi.   Jose Mara naye alitumbuiza. MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo imetibua shoo ya mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee nakusababisha shoo hiyo kusogezwa mbele mpaka itakapotangazwa. Shoo hiyo iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge ambapo mbali na Lady Jay Dee walikuwa wamealikwa wasanii wengine wakiwemo, Prof. Jay, Patricia Hillary, Roma mkatoliki, Baghda...