WANANCHI WATAKIWA KUONGEZA THAMANI MAZAO YA KILIMO
Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia (kulia) akiwa na baadhi ya wakulima wa ufuta wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana, katika banda la Farm Afrika kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijijni Arusha. Watanzania wenye asili ya bara Asia wakipewa maelezo ya ubora wa mafuta ya ufuta kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha. Wakulima wametakiwa kutumia fursa ya kuongeza thamani mazao yao ili waweze kunufaika zaidi kiuchumi kuliko kuuza mazao yao yakiwa ghafi kwani watakuwa wanayonywa na kuzidi kuwa masikini. Wito huo umetolewa jana na Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye maonyesho ya wakulima nane nane, kanda ya kanda ya kaskazini yanayoendelea jijini Arusha. Alisema kupitia Farm Africa wakulima ...