Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA.
Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA.
Siku
ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake
wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga
mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii
na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali
hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa
ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa
wanawake.
Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945,ilipofika tarehe
8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi
huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya
haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa
pekee.
Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha
jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki
mbalimbali za Kimataifa/ kikanda na kitaifa zinazohusu masuala ya
maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha haki za wanawake
kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinapatikana na zinalidwa.
Aidha, kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii
kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa
wanawake katika kuleta maendeleo, kuelezea jitihada mbalimbali
zilizofanywa na Serikali na wadau wengine katika kuwajengea uwezo wa
kiuchumi na kijamii ili waweze kushiriki kikamilifu kujiletea maendeleo
yao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
Tanzania ilianza kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 1996,
maadhimisho yamekuwa yakiandaliwa Kitaifa na katika ngazi ya mkoa.
Hivyo maadhimisho ya mwaka huu 2014 yanafanyika katika ngazi ya
mkoa, na kila Mkoa umeandaa utaratibu wa maadhimisho haya kwa kusisitiza
Kaulimbiu ya kimataifa ambayo ni; “CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA
KIJINSIA”.
Comments
Post a Comment