Posts

Maya: Naitamani sana ndoa na watoto wawili tu!

Image
Maya: Naitamani sana ndoa  na watoto wawili tu! Staa wa ‘long time’ kwenye tasnia ya filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’. K ama kawa, kama dawa! Wiki hii tunaye mwanadada wa ‘long time’ kwenye tasnia ya filamu Bongo. Wengi wanamjua kwa jina la Maya lakini jina lake kamili ni Mayasa Mrisho. Paparazi wetu, Hamida Hassan alikutana naye kitaani na kumbana kwa maswali 10. Natumaini una hamu ya kujua kaulizwa maswali gani na yeye akayajibu vipi, kama jibu ni ndiyo, ungana nami hapa chini… Ijumaa: Mambo mdada, siku hizi umepotea kweli, tatizo nini mamy au umeolewa? Maya: Mh! Una maneno wewe, niko bize na mambo ya biashara ndiyo maana. Kwa filamu sifanyi kivile, nafanya kidogo kisha naendelea na mishe za kusaka noti. Ijumaa: Unadhani ni kwa nini soko la filamu kwa sasa limekuwa gumu kiasi cha kila mtu kusema mambo siyo mambo? Maya: Ni kweli soko limekuwa gumu, sababu ni wizi tunaofanyiwa, filamu feki zipo kibao mtaani, ukitoa filamu yako ikakulipa shukuru...

H-Baba Atahadharishwa Kumzeesha Flora

Image
H-Baba Atahadharishwa Kumzeesha Flora H-Baba, mkewe Flora Mvungi ns mtoto wao. Stori: Hamida Hassan Licha ya H-Baba kudai kuwa, mkewe Flora Mvungi anazidi kuwa mzuri licha ya kuwa mama wa watoto wawili, mashabiki wake wamemtahadharisha kwa kumwambia kuwa, asipoangalia atamzeesha bila kutarajia. Flora juzikati alidaiwa kujifungua mtoto wa tatu na alipotupia mtandaoni picha inayomuonesha akiwa na baby, wengi walimpongeza lakini wapo waliompa H-Baba tahadhari kuwa, anavyombebesha mimba za fasta mkewe atakuwa anamfanya aonekane mmama wakati bado ni binti. “Unajua bwana kila mtu ana uamuzi wake, kitendo cha H- Baba kutaka kupata watoto fasta, siyo kibaya lakini Flora anazeeka yule, muoneni hivi hivi…” alisema mdau mmoja. H- Baba sasa ana watoto watatu ambao ni Tanzania, Afrika na huyo mdogo ambaye taarifa zake hazijaanikwa.

Jichanganye ndani ya Dar Live leo katika Ladies Night

Image
Jichanganye ndani ya Dar Live leo katika Ladies Night

Balaa Jipya Makalio ya Kichina na madhara yake

Image
Balaa Jipya Makalio ya Kichina na madhara yake Stori: Hamida Hassan na Boniface Ngumije D ar es Salaam: Tabia ya baadhi ya wasichana hasa wa mjini kuwa na tamaa ya kuwa na makalio makubwa na hivyo kulazimika kutumia dawa mbalimbali, imekuwa ikishamiri kila siku licha ya serikali kupiga marufuku uingizwaji wa dawa hizo. Jayjay Gazeti hili matoleo yaliyopita liliwahi kuandika jinsi mastaa wengi Bongo wanavyotumia dawa hizo lakini uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, kasi ya matumizi ya dawa hizo yamekuwa yakishamiri huku waathirika wengi wakijiuguza kwa siri baada ya kupata madhara. Gilla . Katika tukio jipya la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hamisa ambaye alidai ni mke wa mtu alisema kuwa, alishawishiwa na rafiki yake kutumia dawa hizo ili naye awe na ‘zigo’ lakini ameanza kuona zinamletea matatizo. “Nimekuwa nikisikia kuwa dawa hizi zina madhara lakini kuna rafiki yangu mmoja ambaye aliwahi kutumia na yuko poa...

Simba kushuka kijeshi, Kaseja azua hofu Mbeya City

Image
Simba kushuka kijeshi, Kaseja azua hofu Mbeya City Wachezaji wa Simba wakifanya yao. Nicodemus Jonas, Dar es Salaam BAADA ya kuwa mafichoni kwa takriban wiki moja mkoani Morogoro, kikosi cha Simba sasa kipo fiti, tayari kuwavaa Mbeya City katika mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Simba wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya lakini Simba ilikuwa chini ya Muingereza, Dylan Kerr wakati kwa sasa ipo chini ya Mganda, Jackson Mayanja. Meneja wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amewahakikishia Wanasimba kuwa kwa mazoezi waliyofanya, wana uhakika wa ushindi. “Kikosi kipo vizuri, bahati nzuri wachezaji karibia wote wapo, isipokuwa Hija Ugando ambaye alibaki Dar akiuguza majeraha, lakini wengine wote wapo kambini katika maandalizi ya mchezo huo,” alisema Gazza. Kipa wa Mbeya City, Juma Kaseja. Aidha, upande wa M...

Kiiza aandikiwa barua ya onyo kali Simba

Image
Kiiza aandikiwa barua ya onyo kali Simba Mshambuliaji wa Simba, Kiiza. Wilbert Molandi na Hans Mloli KATIKA kuhakikisha wanatengeneza nidhamu kwenye timu, uongozi wa Simba umeliagiza Benchi la Ufundi la timu hiyo kumuandikia barua ya onyo kali mshambuliaji wake Mganda, Hamis Kiiza. Hatua hiyo imekuja siku chache tangu uongozi wa Simba utangaze kumsimamisha beki na nahodha wake msaidizi, Hassani Isihaka kwa kile kilichodaiwa kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kocha wao Mganda, Jackson Mayanja. Mara ilivyotangazwa kusimamishwa kwa Isihaka, Kiiza alimtetea beki wake huyo katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kiliwakasirisha viongozi wa Simba. Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa tayari wamemuagiza meneja wa timu hiyo, Abbas Ally kumuandikia barua ya onyo mshambuliaji huyo. Taarifa kutoka ndani ya kambi ya Simba iliyopo Morogoro imeeleza kuwa Kiiza aliomba radhi kwa al...

Mgombea wa Urais Marekani Donald Trump Ashutumiwa Kuwa ni Tapeli...Atakiwa Kukatwa katika kinyanganyiro cha nafasi ya urais.nchini marekani

Image
Mgombea wa Urais Marekani Donald Trump Ashutumiwa Kuwa ni Tapeli...Atakiwa Kukatwa Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Mitt Romney amekitaka chama chake kumkataa Donald Trump ,akimtaja mgombea huyo aliye kifua mbele kuwa ”tapeli”. Bwana Romney amemshtumu Bwana Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani kama wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari. Bwana Trump hatahivyo amemkejeli bwana Romney katika mtandao wa tweeter kama mgombea aliyefeli na ambaye hafai kutoa ushari wowote kuhusu uchaguzi. Viongozi wakuu wa chama cha Reupblican wameshangazwa na vile bwana Trump anavyoelekea kushinda tiketi ya chama cha Republican kwa uchaguzi huo wa mwezi Novemba. Inadaiwa kuwa wanachama kadhaa wa kamati ya kitaifa kuhsu usalama wa jamii waliandika barua ya wazi wakielezea maono ya bwana Trump kama yasio na msingi wala sera. Bwana Trump amejiwasilisha kama muunganishi kufuatia ushindi wake katika majimbo saba katika il...