Maya: Naitamani sana ndoa na watoto wawili tu!
Maya: Naitamani sana ndoa na watoto wawili tu!
Kama kawa, kama
dawa! Wiki hii tunaye mwanadada wa ‘long time’ kwenye tasnia ya filamu
Bongo. Wengi wanamjua kwa jina la Maya lakini jina lake kamili ni Mayasa
Mrisho.
Paparazi wetu, Hamida Hassan
alikutana naye kitaani na kumbana kwa maswali 10. Natumaini una hamu ya
kujua kaulizwa maswali gani na yeye akayajibu vipi, kama jibu ni ndiyo,
ungana nami hapa chini…
Ijumaa: Mambo mdada, siku hizi umepotea kweli, tatizo nini mamy au umeolewa?
Maya: Mh! Una maneno
wewe, niko bize na mambo ya biashara ndiyo maana. Kwa filamu sifanyi
kivile, nafanya kidogo kisha naendelea na mishe za kusaka noti.
Maya: Ni kweli soko
limekuwa gumu, sababu ni wizi tunaofanyiwa, filamu feki zipo kibao
mtaani, ukitoa filamu yako ikakulipa shukuru Mungu.
Ijumaa: Vipi suala la kuwa na familia maana naona umri unasonga na hatusikii cha ndoa wala mtoto.
Maya: Kila mtu ana
maamuzi yake, kiukweli natamani kuolewa na naamini ipo siku Mungu
atanibariki katika hili. Nina hamu ya kuwa mke wa mtu na nikipata watoto
wawili nitafurahi sana.
Ijumaa: Suala la mastaa kushea mabwana siyo geni na mastaa kugombea mwanaume imekuwa ikitokea sana, wewe ushafikia hatua hiyo?
Maya: Mimi najitambua
sana, siwezi kugombea mwanaume wala kutembea na mtu ambaye ana mtu wake
maana kufanya hivyo ni kujitafutia matatizo.
Ijumaa: Uliwahi kuwa na uhusiano na msanii mwenzako, jina nalihifadhi, sababu za kuachana naye ni zipi?
Maya: Mh! Naomba sana hilo swali nisilijibu, please!
Ijumaa: Inadaiwa kufariki kwa Kanumba kumekuathiri kiasi cha kutofanya filamu, tangu ameondoka umecheza filamu ngapi?
Maya: Kuondoka kwake ni pigo lakini nimefanya filamu nyingi tu. Ni mwaka wa nne tangu afariki hivyo nisingeweza kukaa bila kuigiza.
Ijumaa: Mtu akikupa ofa ya kukutoa ‘out’ unapendelea kwenda sehemu gani?
Maya: Napenda sehemu yoyote ile iwe imetulia tu, huo ndiyo ugonjwa wangu, sipendi sehemu zenye kelele.
Ijumaa: Ni msanii gani unadhani anaweza kufuata nyayo za Kanumba?
Maya: Sijaona msanii anayefuata nyayo zake, kama unavyojua alikuwa mpiganaji na aliweza kutanua soko nje na ndani.
Ijumaa: Mastaa wengi wenye makalio wanadaiwa kutumia dawa za Kichina, inadaiwa na wewe ni mmoja wao, unalizungumziaje hilo?
Maya: Hiyo kali, kiukweli sijawahi hata siku moja kutumia dawa hizo maana najua zina madhara ya baadaye.
Ijumaa: Unawazungumziaje wasanii wenzako wanaoifanya tasnia ya filamu kama kichaka cha kufanyia ufuska?
Maya: Kikubwa ni kubadilika tu, tukijiheshimu na sisi tutaheshimika. Skendo huwa zinatufanya tudharaulike.
Comments
Post a Comment