BABY MADAHA ANUSIRIKA KUBAKWA

Tukio hilo lilitokea pande za Mombasa nchini Kenya wakati nyota huyo alipokuwa akirekodi video ya wimbo wake uitwao The Gal Bladder ambapo vijana hao walikatisha shughuli nzima na kuanza kumkimbiza Baby Madaha.
“Daah! Ilikuwa noma, ilikuwa usiku sasa wakati meneja wangu akinielekeza matakwa ya video hiyo ambayo yalihitaji vijana wa mtaani, ghafla wakatokea vijana wenyewe wa mtaani na kutaka kunibaka. Bahati nzuri nilifanikiwa kutimua mbio na kuwazidi,” alisema Baby.
Comments
Post a Comment