Maelfu wamzika Mzee Nelson Mandela kijijini kwao Qunu leo
Maelfu wamzika Mzee Nelson Mandela kijijini kwao Qunu leo
Mazishi
ya Nelson Mandela yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa
Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa
Afrika,Nelson Mandela.
Takriban
watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo
ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
Familia
ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na
muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia
wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni
kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu.
Viongozi
wa Afrika, familia na marafiki wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati
Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu
katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo
wa Afrika Kusini.
Rais
Jacob Zuma amesema kuwa wakati safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru
imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na
urithi wake.
Comments
Post a Comment