BAADA YA WEMA SEPETU KUPEWA 'NOTICE' YA KUHAMA KATIKA NYUMBA ANAYOISHI...SASA DIAMOND KUMNUNULIA NYUMBA YA TSH.125 MILIONI
BAADA YA WEMA SEPETU KUPEWA 'NOTICE' YA KUHAMA KATIKA NYUMBA ANAYOISHI...SASA DIAMOND KUMNUNULIA NYUMBA YA TSH.125 MILIONI
Nasibu
Abdul ‘Diamond’ anadaiwa yuko kwenye mchakato wa kumnunulia jumba la
kifahari mpenzi wake wa ‘nenda rudi’, Wema Sepetu, Amani limeinyaka hii.
![]() |
Nasibu Abdul ‘Diamond’ |
Kwa
mujibu wa chanzo, Diamond ameamua kuingia kwenye kujikamua huko kufuatia
taarifa kwamba, mmiliki wa nyumba anayoishi Wema kwa sasa (jina lipo),
Kijitonyama, Dar es Salaam amemwamuru mlimbwende huyo kuhama kwenye
mjengo wake mara baada ya kumaliza mkataba mwezi Juni, mwaka huu. Awali
mjengo huo aliutangaza ni wake.
![]() |
Wema Sepetu |
“Mwenye
nyumba anayoishi Wema kwa sasa amekataa mrembo huyo kuendelea kuishi
pale, akimaliza mkataba wake Juni, mwaka huu basi, hataki tena.
“Sasa
Diamond aliposikia hilo akamwambia Wema isiwe tabu, akamuahidi
kumnunulia nyumba ya kifahari yenye thamani ya shilingi milioni mia moja
na ishirini na tano.
“Nadhani hiyo nyumba ipo tayari, ndiyo maana amemtajia na bei. Lakini ninavyojua mimi ipo Mwananyamala,” kilisema chanzo.
“Nadhani hiyo nyumba ipo tayari, ndiyo maana amemtajia na bei. Lakini ninavyojua mimi ipo Mwananyamala,” kilisema chanzo.
Kuhusu
nyumba ya sasa, ni kweli ‘kifo cha nyani miti yote huteleza’ kwani Wema
anatakiwa kutoendelea na mkataba mpya ikiwa ni siku chache tu baada ya
Mahakama ya Ilala, Dar es Salaam kuamuru anyang’anywe lile gari lake la
kifahari aina ya Audi Q7 lenye usajili wa T 973 BUJ na kukabidhiwa
mmiliki wake halali, Shadrack Tweve.
Wema
alipewa gari hilo na mwanaume anayedaiwa ni mpenzi wake anayejulikana
kwa jina la Clement ambaye alilikopa kwa mmiliki huyo lakini alikuwa
akikwepa kulipa deni la shilingi milioni 90.
Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar, mmoja wa ‘kruu’ ya Wema ambaye hakutaka jina lake lionekane gazetini alisema kwa sasa Wema yuko katika kipindi kigumu baada ya kumwagana na kigogo huyo aliyekuwa akidaiwa kumpa jeuri na kufuatia kuamriwa kuhama kwenye nyumba hiyo.
Chanzo chetu kikazidi kumwaga data kuwa mbali na Wema kuachana na Clement, bado mrembo huyo amekuwa katika kipindi kibaya zaidi baada ya kunyang’anywa gari hilo ambalo ndilo alilokuwa akilitumia.

Comments
Post a Comment