Skip to main content
HIZI NDIZO DALILI ZA MWANAMKE:HIZI NDIO DALILI KWAMBA MWANAUME ULIYE NAYE SI WAKO PEKE YAKO!!!!
HIZI NDIZO DALILI ZA MWANAMKE:HIZI NDIO DALILI KWAMBA MWANAUME ULIYE NAYE SI WAKO PEKE YAKO!!!!

Wakati mwingine ni vigumu kuamini, lakini jambo hili huwatokea wanawake
wengi kwamba wanaume wanaotoka nao kuna uwezekano mkubwa wakawa wanatoka
na wanawake wengine kwa nyakati tofauti na hufanya hivyo kwa siri sana.
Inaweza ikawa ni mitoko ya kawaida lakini miongoni mwa hao wanaotoka
nao wapo ambao watakuwa wanashiriki tendo na wakawa wameahidiwa kuolewa.
Hapa chini nitaeleza dalili zinazoweza kuwafanya wanawake kujua kwamba
mwanaume anayetoka naye sio wakwake peke yake bali kuna wengine
wanadanganywa huko waliko kama yeye.

1. Mnakuwa na ratiba ya kukutana siku maalum
Baada ya kujuana unagundua kwamba bwana uliye naye anakuwa na kawaida ya
kukutana na wewe kwa siku maalum tena anazopanga yeye, mwanaume anakuwa
hana nafasi ya kushtukizwa miadi na akipanga ratiba yake hawezi
kuibadilisha kirahisi. Anaweza kukupangia muwe mnakutana mara mbili kwa
wiki na siku nyingine anasema yuko bize. Hapa inabidi ujiulize mara
mbili.

2. Ugumu katika kukubali miadi:
Kama inatokea unamuomba mkutane kwa ajili ya mtoko siku fulani ni vigumu
kukubali ombi hilo mara moja, sana sana ataishia kusema, "Inawezekana
lakini sina uhakika" au "nitaangalia kama nitakuwa na nafasi." Pamoja na
kutotoa jibu la kukubali moja kwa moja, lakini hatakuwa na sababu
yoyote ya msingi ya kutokubali mualiko huo moja kwa moja. Mara nyingi
wanajiumauma tu. Ukiona hivi akili kichwani mwako.

3. Usiri na kutokuwa wazi:
Kama mwanaume anatokea kumpenda mwanamke na anamatarajio ya kufika mbali
na yeye, kwa maana kwamba huenda akafunga naye ndoa, atakuwa muwazi
kwake hususan kuhusu maisha yake binafsi na shughuli zake. Lakini kama
mwanaume akionekana kutokuwa muwazi na mtu anayeficha ficha kuhusu
maisha yake na mambo yake, basi jua kwamba atakuwa na mwanamke mwingine
anayetoka naye hivyo anaogopa kuweka mambo yake wazi ili asije akaharibu
upande wa pili. Hapa mwanamke inabidi awe na akili kumkichwa.

4. Msururu wa marafiki wa kike:
Kwa kawaida wanaume wasiotulia wanakuwa na msururu wa marafiki wa jinsia
ya kike, na huwa wanadai kwamba hao ni marafiki zake tu na hakuna jambo
lolote zaidi ya urafiki wa kawaida, lakini kumbe ni urafiki
unaomnufaisha kingono (friends with some benefits). Wanaume wenye
kupenda kuzungukwa na wanawake wanakuwa katika nafasi nzuri ya kutoka
nao kimapenzi hivyo huo mtego hauwezi kuwakosa na kama inavyojulikana
kwamba wapo baadhi ya wanawake hupenda kutoka na wanaume wasiotulia,
unadhani ataepuka mtego wao. Hivyo ukiona mwanaume ana msururu wa
marafiki wa kike iwe ni wale anaokutana nao au wale wa kwenye mtandao,
jua huko peke yako......
5. Uzuri wa kubembeleza na lugha tamu:
Wanaume wasiotulia wanajua sana kubembeleza na wanakuwa na lugha tamu
ambayo huwavutia wanawake, ni wazuri sana katika mazungumzo na ni rahisi
kuteka hisia za mwanamke yeyote amtakaye. Mara nyingi ni rahisi
kuwanasa wanawake wapendavyo kwa sababu wanajua sana kubembeleza na
kujali hisia za wanawake. Lakini hata hivyo siyo wanaume wote wenye
haiba hiyo kwamba hawajatulia, bali baadhi hutumia haiba hiyo kuwanasa
wanawake kiurahisi. hapa nashauri tu mwanamke achunguze kwa makini kabla
ya kutuhumu eti kwa sababu Mtambuzi kasema.......

6. Kushtukiza mitoko:
Wanaume wasiotulia mara nyingi wanakuwa ni mabingwa wa kushtukiza mitoko
(dates) pale ambapo mwanamke hatarajii kutoka hushtukizwa kwa simu au
ujumbe mfupi wa simu kwamba ajiandae kwa mtoko na akiuliza mbona imekuwa
ghafla hivyo jibu lake litakuwa ni rahisi tu, "It is Suprise" Nilikuwa nataka kukushangaza tu. Na kwa kuwa wanakuwa na lugha tamu, nirahisi kubembeleza na kukubaliwa huo mtoko.

7. Tatizo la kutunza kumbukumbu:
Siyo kila mtu anaweza kuwa na kumbukumbu nzuri, lakini kwa kawaida kama
unamjua mtu fulani, ni lazima kuna kumbukumbu zitakujia kuhusu tabia
zake na vitu vinavyomhusu mtu huyo. Lakini kama inatokea kila unapokuwa
na mwanaume unayetoka naye anakusimulia stori hiyo hiyo kila mnapokutana
na kukuliza maswali yale yale anayokuuliza kila mnapokutana pamoja na
kwamba umekuwa ukimjibu mara kwa mara na anakuwa na na matatizo ya
kuweka kumbukumbu, jua kwamba huko peke yako kuna wanawake wengine
anatoka nao hivyo hakumbuki stori ipi alimsimulia nani au aliwahi
kukuuliza swali hili au la.........

8. Kukuchukulia kama rafiki tu:
Hii ni dalili mojawapo ambayo haina mjadala, pale ambapo mwanaume
unayetoka naye anakuchukulia kama rafiki na siyo mpenzi wako, hususan
pale anapokuwa na marafiki zake au kama mwanaume unayetoka naye hakuiti
mpenzi, au hakutambulishi kwa marafiki zake kama wewe ni mpenzi wake
basi jua kwamba anao msururu wa wanawake anaotoka nao hivyo anaogopa
kuwachanganya marafiki zake na kuonekana kama hajatulia. Inama chini
ufikiri.............

9. Ni vigumu kutimiza ahadi:
Kwa kawaida wanaume wana kawaida ya kusema jambo lolote ambalo wanajua
litamvutia mwanamke, Wengi wao hupenda kuahidi mambo makubwa, lakini
tatizo ni utekelezaji wa ahadi hiyo. Anaweza kumuahidi mwanamke kumpa
zawadi aliyokuwa akiitamani au kumpeleka visiwani kwenye hoteli za
kitalii kwa ajili ya kujipumzisha na kuponda raha, lakini ahadi hizo
zitaendelea kuwa hadithi za Alinacha. Wanaume wasiotulia wanakuwa ni
mahiri sana wa kutumia lugha laini kuwalainisha wanawake, hilo tu na si
vinginevyo........

10. Mapenzi kwa mgao:
Huwezi kujua kama tendo litafanyika au halitafanyika, hata kama mkiwa
mmejifunika shuka moja kitandani. Kuna wakati Tendo hufanyika kwa
umahiri mkubwa mpaka unajisikia raha, lakini kuna siku ambayo kutokana
na mazingira unaweza kujua kwamba gwaride litachezwa, lakini ukaambulia
kapa. basi hapo jua kwamba, kuna mwanamke mwingine mahali fulani ana
miadi ya kukutana naye hivyo anakwepa ili kukusanya nguvu za kutumika
kwingine.
Comments
Post a Comment