Posts

Showing posts from February, 2014

MATUKIO : DIWANI WA KATA YA SOMBETINI MHE. ALLY BANANGA AKARIBISHWA OFISINI

Image
MATUKIO : DIWANI WA KATA YA SOMBETINI MHE. ALLY BANANGA AKARIBISHWA OFISINI Diwani Mteule Mhe. Ally Bananga akisaini kitabu cha wageni ofisini Manispaa ya Jiji la Arusha, na Mhe. Ephata Nanyaro Diwani wa Kata ya Levolosi (pembeni kushoto) kwa nyuma ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema. Afisa Utumishi Manispaa ya Jiji la Arusha akitoa somo kwa Diwani mteule wa Sombetini Mh Ally Bananga (hayupo pichani). Mhe. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini akimsindikiza Mhe. Ally Bananga (Diwani Mteule Kata ya Sombetini ) Mh Ngowi Mbunge viti Maalum Kilimanjaro akisaini kitabu cha wageni, nae alimsindikiza Diwani Mteule Mh.Ally Bananga. Kwa picha Zaidi bofya hapa >>>

TEKNOLOJIA NA MABADILIKO YAKE: WAZIRI DKT. FENELLA MUKANGARA AFUNGUA LA 9 LA CTO LA MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI (DBSF) JIJINI ARUSHA

Image
TEKNOLOJIA NA MABADILIKO YAKE: WAZIRI DKT. FENELLA MUKANGARA AFUNGUA LA 9 LA CTO LA MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI (DBSF) JIJINI ARUSHA    Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akifuatilia hotuba mbalimbali katika ufunguzi wa Kongamano la 9 la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda dijitali Afrika  2014 (DBSF)ulioanza jijini Arusha. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano kwa nchi za Jumuia ya Madola (CTO), Tim Unwin akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John S.Nkoma. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John S.Nkoma akitoa hotuba yake.  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John S. Nkoma akizungumza. Baadhi ya waalikwa ambao ni viongozi wa Vituo vya televisheni nchini Tanzania  Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Wakuruge...

MAZISHI : LOWASSA ASHIRIKI MSIBA WA PATRICK QORRO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
MAZISHI : LOWASSA ASHIRIKI MSIBA WA PATRICK QORRO JIJINI DAR ES SALAAM Mh Lowassa an mkewe mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho ka mwili wa marehemu comrade Mbunge  wa zamani wa Karatu comrade Patrick Qorro Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimsalimia waziri mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Jaji Joseph warioba katika msiba wa mbunge wa zamani wa Karatu Patrick Qorro ,Ada Estate Dar es Salaam.  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimsalimia Prof. Issa Shivji Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku katika msiba wa mbunge wa zamani wa Karatu Patrick Qorro jijini dsm leo hii Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ni Waziri Mkuu Msataafu na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wakiondoka eneo la msiba. ...

USIHANGAIKE : MAFOTO PRODUCTION & ENTERTAINMENT

Image
USIHANGAIKE : MAFOTO PRODUCTION & ENTERTAINMENT MAFOTO PRODUCTION & ENTERTAINMENT KWA MAHITAJI YAKO YA STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING, MUSIC & Mc’s KATIKA SHEREHE YA AINA YEYOTE.  KAZI NYINGINEZO:- VIDEO EDDITING, COVER DISGNING, PPS ZA DK 3, POSTERS ZA AINA MBALIMBALI COVER CD PRINTING, BURNING CD N.K. WASILIANA NASI KWA NO, 0787 200005/0754, 0655-306109/0714 656660    BARUA PEPE:- muhidinuk@yahoo.co.uk,sufianimafotoblog@gmail.com AMA TEMBELEA www.sufianimafoto.com   OFISI ZETU ZIPO KIJITONYAMA NYUMA YA KITUO CHA POLISI MABATINI, BARABARA YA SPIKA WA BUNGE

URAFIKI KIMATAIFA :KAMISHNA WA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA ATEMBELEA MAGEREZA TANZANIA

Image
URAFIKI KIMATAIFA :KAMISHNA WA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA ATEMBELEA MAGEREZA TANZANIA   Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (wa nne kulia) akiwa na  Jenerali wa Magereza Tanzania John Minja (katikati)  wakimsiliza kwa makini Mnadhimu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mmeta Manyara akijitambulisha. Kamishna Chato  ametembelea Makao Makuu ya Magereza ikiwa kni ziara ya siku sita nchini Tanzania.Wa tatu kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Yumbe, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Tebuho Nyambe na wa kwanza ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza James Nkoloma wote kutoka Makao Makuu ya Magereza nchini Zambia. Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato ( wa nne kushoto), akipokea taarifa fupi kutoka kwa mmoja wa maofisa  kiwandani Ukonga. Kamishna Percy alitembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga, Dar es salaam kuona shughuliza za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanyika. Kamishna wa ...

HAYA NAYOMATATIZO YANAYOKUMBA NDOA NA KAZI KWA KILA MWANA NDOA HILI NALO NENO...: LADY JAY DEE AOMBA TALAKA KUTOKA KWA MUME WAKE

Image
HAYA NAYOMATATIZO YANAYOKUMBA NDOA NA KAZI KWA KILA MWANA NDOA HILI NALO NENO...: LADY JAY DEE AOMBA TALAKA KUTOKA KWA MUME WAKE Stori:  Shani Ramadhan UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo kuomba aandikiwe talaka, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuripoti mkasa wote. Jide akiwa na mumewe Gardner. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Jide au Lady Jaydee alifikia uamuzi huo baada ya Gardner kupata kazi ya kutangazia redio moja nchini Kenya. HABARI KAMILI Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa mara baada ya mume huyo kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati hiyo. “Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbi...

WANAWAKE WANAWEZA: UN WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUWAENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII

Image
WANAWAKE WANAWEZA: UN WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUWAENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII Pichani ni  Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo wakinamama wamekuwa wakifanya kwa mustakabali kwa kuleta usawa na haki za wanawake duniani. Shirika la Ufaransa la Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya maonyesho iliyopewa jina “women in Resistance by the talented French photo-journalist Pierre-Yves Ginet. Mwandishi wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakinamama wengi Afrika. Kati ya 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama ambayo katika shug...

MABOMBA YA GESI YASHUSHWA :NAIBU WAZIRI MHE. KITWANGA APOKEA SHEHENA YA MWISHO YA MABOMBA YA GESI BANDARI YA MTWARA.

Image
MABOMBA YA GESI YASHUSHWA :NAIBU WAZIRI MHE. KITWANGA APOKEA SHEHENA YA MWISHO YA MABOMBA YA GESI BANDARI YA MTWARA. Naibu Waziri Mhe. Charles Kitwanga (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, (wa kwanza kulia) wakipata   maelezo kutoka kwa mtaalamu Abshakim Marunda kuhusu namna kisima cha  gesi cha nchi Kavu kinavyofanya kazi.  Kwa mujibu wa Maelezo ya Mjiologia Mwandamizi wa TPDC Bw.George Ngwale hayupo pichani ameeleza kuwa, Mnazi Bay ina jumla ya visima vitano kati ya hivyo visima vine vina gesi  inayochimbwa na kisima kimoja kikavu.  Aidha gesi inayopatikana katika  eneo hili inauzwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao wanatumia  kuzalisha umeme unaosambazwa katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Wa kwanza  kushoto ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri Bw. Mjengwa Ngereja. Na Asteria Muhozya, Mtwara Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayesh...

UKATILI WA KIJINSIA : MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA MPENZI WAKE KWA KUKATAA KUTOA PENZI

Image
UKATILI WA KIJINSIA : MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA MPENZI WAKE KWA KUKATAA KUTOA PENZI Jeneza la Marehemu, Sekunda Mushi (42), aliyeuwawa kinyama usiku wa kuamkia, Januari 6, wakiwa na majonzi katika mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kuuwa kwa sababu ya kimapenzi baada ya kuibuka kwa ugomvi kati yake na Mpenzi wake, aliyetajwa kwa jina la Gerald Mamkwe. Jeneza la mwili wa Marehemu Sekunda Mushi likiingizwa kaburini katika maziko yaliyofanyika jana katika kijiji cha Longuo A, kata ya Uru Kusini, manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Baba mzazi wa Sekunda Mushi (mwenye suti Nyuesi), akisikliza mahubiri ya mwisho katika ibada ya maziko ya mwanae, Sekunda Mushi, aliyeuwawa kikatili usiku wa kuamkia Januari 6 katika kile kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi. Mzee Onesmo Mushi, ambaye ni Baba Mzazi wa Marehemu Sekunda Mushi, akiweka udongo katika kaburi la mwanamke huyo aliyeuwawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, kutokan...