WANAWAKE WANAWEZA: UN WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUWAENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII
WANAWAKE WANAWEZA: UN WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUWAENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII
Pichani
ni Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves
Ginet akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za
jijini Dar es Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa ufafanuzi wa mambo
mbalimbali ambayo wakinamama wamekuwa wakifanya kwa mustakabali kwa
kuleta usawa na haki za wanawake duniani.
Shirika
la Ufaransa la Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya
maonyesho iliyopewa jina “women in Resistance by the talented French
photo-journalist Pierre-Yves Ginet.
Mwandishi
wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya
kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi
zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakinamama wengi Afrika.
Kati
ya 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama
ambayo katika shughuli zao waliweza kufungua ukurasa mpya na
kubadilisha historia katika kizazi cha leo.
Katika
shughuli na katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha
wa wakinamama wengi duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet
wameweza kuwa na dhamira moja kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili
kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi kwa sasa na baadaye.
Maonyesho
hayo ya lengo la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa
duniani na hasa nchi zinazoendelea, sehemu za vita.
Na
sehemu kubwa ya picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana
ili kujikwamua katika unyonge na ukandamizaji wa aina yoyote hapa
duniani.
Mmoja
wa wananfunzi akibadilishana mawazo na Mwandishi wa habari na mpiga
picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet anayetumia maonyesho ya picha
mbalimbali kuelimisha jamii kupitia picha hizo.
Afisa
Habari kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia
Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari
mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.
Ujumbe
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika kuadhimisha siku ya kimataifa
ya kupinga ukeketaji duniani inayoambatana na siku ya Wanawake Duniani
ni kufikisha sifuri katika kuondoa swala ukeketaji duniani.
Ujumbe
unasema kwamba ukeketaji umepungua katika sehemu kubwa ya dunia na
takwimu zinasema kwamba zaidi ya wanawake na wasichana 125 milioni ambao
wanaishi katika dunia ya leo katika nchi 29 za Afrika na Mashariki ya
kati walifanyiwa vitendo vya ukeketaji, na kama swala hii likiendelea
zaidi ya wasichana 86 milioni duniani watafanyiwa vitendo vya ukeketaji
kufikia mwaka 2030.
Salome
Anyoti kutoka shirika la umoja wa mataifa la wanawake akisisitiza jambo
kwa wanafunzi wa sekondari wa kutoka shule mbalimbali hapa Dar es
Salaam katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuangali picha za
wakinamama walioleta mabadiliko katika maisha yao na wengine kwa
ujumla.
Hizi ni baadhi ya picha za wanawake nchini Tanzania ambao wameleta mabadiliko katika maisha yao na wengine hapa nchini.
Baadhi
ya picha zinazoonyesha matukio mbalimbali yaliyokusanywa na Mwandishi
wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet. Kwa picha
zaidi bofya hapa >>>
Comments
Post a Comment