HATIMAYE KIONGOZI MARKIA NA RAIS MPYA WA KIJIJI CHA MAISHA PLUS WAPATIKANA
Rais Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Mary Masha kutoka Nchini Kenya
Ndani ya Kijiji cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula kila siku
ya Alhamisi huwa panafanyika uchaguzi wa kumpata Rais mpya ambaye
anachaguliwa na Washiriki wenyewe wa Kijiji cha Maisha Plus ambapo kati
ya hao mmoja hupatikana na Marais waliopita hawapatiwi nafasi ya
kugombea tena, na kwamba mama yake na Rais huteuliwa moja kwa moja kuwa
Markia wa Kijiji hicho.
Kazi ya uchaguzi ilianza Kijijini hapo ambapo idadi ya washiriki 36
wakiwemo vijana 16 na kinamama 20 Kila siku ya Alhamisi ni siku ya
uchaguzi wa Rais wa kijiji cha Maisha Plus ambaye husimamia shughuli
zote zinazofanyika katika kijji hicho.
Wiki hii washiriki 10 waliteuliwa kugombea nafasi ya urais ambapo 7
ndiyo waliopigiwa kura ya siri na kupata mshindi. Washiriki wawili kati
yao hawakuweza kugombea nafasi ya hiyo kutokana na utaratibu uliopo
kwamba aliyewahi kushika wadhifa huo kwa muhula uliopita hataweza
kugombea tena.
Marais hao wa mihula uliyopita ni Bonifas Mang’anyi na Bakari
Khalid wote watanzania. Abdul Karim kutoka Burundi alijitoa kwa kuwa
hakuwa tayari kushika wadhifa huo kwa sasa.
Kwa kawaida kila kijana huwa na mama katika kijiji cha Maisha Plus
na endapo kijana atachaguliwa kuwa Rais mama yake huwa Malkia ambaye
humshauri Rais na kufanya maamuzi katika kijiji hicho.
Uchaguzi ulifanyika kwa wagombea 7 akiwemo Shida Mganga, Seif
Mohamed, Ally Thabiti, Mbonimpaye Nkoronko na Hyasinta Hokororo kutoka
Tanzania, Ngabozinza Daniel kutoka Rwanda na Mary Masha kutoka Kenya.
Uchaguzi wa Rais ulifanyika mara mbili kwa kuwa washindi walipata kura
sawa iliyopelekea kurudia kupiga kura ili kupata mshindi mmoja.
Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.
Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.
Utaratibu wa kuchagua wagombea: Kila mshiriki hujaza fomu kuteua
jina la atakayekuwa kuwa Rais wa wiki hiyo. Walioteuliwa hujinadi ili
wapate kupigiwa kura na hatimaye kupata mshindi.
Comments
Post a Comment