Je Van Gaal ataumaliza msimu vizuri? Aiongoza United kushinda mechi ya 4 mfululizo

Mapema wiki iliyopita hakuna shabiki wa ambaye alikuwa anaamini timu
yake ingeweza kupata matokeo chanya katika mechi 4 zilikuwa zinafuatana
mfululizo za michuano tofauti, kutokana kiwango cha timu yao na udhaifu
wa kikosi hicho kilichojaa majeruhi.
Lakini chini ya kocha ambaye anaripotiwa kwamba siku zake za
kuendelea kuwa mkufunzi mkuu wa timu hiyo zinahesabika – Manchester
United imefanikiwa kushinda mechi zote zilizokuwa mbele yao.
Baada ya kufungwa 2-1 na FC Mityjlland wiki mbili zilizopita, United
waliifungua wiki iliyopita na ushindi wa 3-0 dhidi ya Shrewbury FC
katika mchezo wa raundi ya 5 ya kombe la FA.

Alhamisi
ya wiki iliyopita Van Gaal na vijana wake wakawa na mtihani wa kugeuza
matokeo ya 2-1 dhidi ya FC Mityjlland baada ya kufungwa nchini Denmark –
na kwa bahati mbaya majeruhi yakazidi kuongezeka, mshambuliaji tegemeo
Antonio Martial akaumia wakati akipasha misuli kabla ya mchezo. Nafasi
yake akapewa kinda kikosi cha pili Marchs Rashford ambaye aling’ara
usiku huo kwa kufunga magoli katika ushindi 5-0 dhidi ya klabu hiyo ya
kidenishi.

Mtihani
uliofuatia ulikuwa jumapili iliyopita dhidi ya Arsenal ambao waliingia
kwenye mchezo huo wakipewa nafasi kubwa ya kushinda baada ya kuitandika
United iliyo kamili 3-0 katika mchezo wa kwanza, alikuwa yule yule
kijana wa Marcus Rashford akapiga tena mbili na Hererra akafunga lingine
na kuwapa United ushindi wa 3-2 na kuamsha ndoto za Van Gaal kumaliza
ndani ya Top 4.
Mechi ya 4 ilikuwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Watford katika mfululizo wa ligi kuu ya England.

Goli
pekee la Juan Mata katika dakika za lala salama liliwezesha United
kufikisha pointi sawa na Manchester City ambao wana pointi 47 katika
msimamo wa ligi.

Matokeo
ya leo yamezidi kuwatia nguvu United na kuamini sasa wanaweza kupambana
na kufanikiwa kumaliza ndani ya nafasi 4 za juu ili kupata nafasi ya
kucheza kwenye Champions League.
Comments
Post a Comment