SERIKALI YATOA MOTISHA KWA WACHEZAJI WA TWIGA STARS
SERIKALI YATOA MOTISHA KWA WACHEZAJI WA TWIGA STARS
Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia James Wambula alipotembelea kambi ya Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao.
Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi yake dhidi ya Zimbabwe kila mchezaji atapata gawio la sh. Laki tatu kama mptisha na kuongeza kuwa itafanyika hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Zimbabwe.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na kuisaidi timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mechi ya tarehe 4 machi dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa katika uwanja wa Taifa.
Aliongeza kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji yake muhimu,hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga Specila Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House jijjini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesiga ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi.
Mwesiga pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo amesema kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza morali ya wachezaji.
Msaada huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu ambapo mmja aliyechangia sh. Milioni 3 aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS sh. Milioni 2 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) sh. Milioni 10.
Imetolewa na habari.go.tz
Comments
Post a Comment