Posts

Mkuu wa Wilaya Lucy Mayenga Aihofia Kasi ya Magufuli..Ajisalimisha na Kumuomba Rais Asimchague Tena Ukuu wa Wiliya

Image
Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote. Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti. Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zin...

Mashabiki Watafsiri Zari ana Mimba Baada ya Mdogo wake Diamond Kudaiwa Kuandika Ujumbe Huu

Image
Wakati Diamond yupo Ujerumani kwa ajili ya tour yake ya Ulaya, Jumatano hii katika mitandao ya kijamii hasahasa instagram kunasambaa ujumbe ambao mashabiki wengi wa Diamond wameutafsiri Zari ana mimba nyingine ya Diamond. Mtangazaji wa U heard ya XXL ya Clouds FM, Soudy Brown, alipost picha ya ujumbe huo na kuandika: Doh Blaza kishaloweka kwa Mara nyingine, haya T subiri mdogo wako on ze way. Sudy Baada ya ujumbe huo mashabiki wa Diamond amekuwa na maoni tofauti juu wa swala hilo. Nurashammy Safi sana Diamond waseme tena furaha mpaka nalala naviyato kwakwei kusikiya kama @zarithebosslady najuwa @diamondplatbumz haukosi kitu ila mimi kama shabiki wako ningependa kutowa zawadi ya tiffah Tajibetese Hivi nikweli naweza kufa kwa furaha @diamondplatnumz @zarithebosslady Nurashammy Safi sana @diamondplatnumz kusikiya kama @zarithebosslady ni mama kijacho ju yafuraha nalala na viyato kwakweli Mungu awape riziki Mchagga_wa_mashati Sijui na hii wata...

RC Paul Makonda Amtembelea Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Ili Kupata Baraka Zake

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao  ambapo jana alimtembelea  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  kwa  ajili  ya  kupata  baraka  na  busara  zake Siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam. Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya kisasa. Akizungumza jana, alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuchukua busara kutoka kwa wazee ili zimsaidie katika utendaji wake. “Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa ...

Zari wa Diamond Adaiwa Kumpa Makavu Laivu Kajala habari kamili ipo apo chini

Image
Kufuatia madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa na katabia ka’ kujiweka kimahaba kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa Sauzi, madai yametua mezani mwa gazeti hili kuwa, kimenuka kati ya Zari na Kajala. Chanzo chetu makini ambacho kimeomba jina lake lisitajwe gazetini kimedai kuwa, hivi karibuni baada ya Zari kupata ubuyu huo wa kuchovyewa penzi lake, alitafuta simu ya Kajala kisha kumpigia na kumpa makavu kuwa, asimuingilie kwenye himaya yake. “Siku moja nilikuwa na Kajala, mara ikaingia simu ambapo alipopokea akasikia sauti ya Zari, basi unaambiwa akamsema sana juu ya kuingilia penzi lake, Kajala akawa kimyaa, wala hajajibu lolote, inavyoonekana alipewa makavu,” alidai mtoa habari huyo. Baada ya kupata habari hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kajala ili kuzungumzia madai hayo ambapo alipokea simu na kupewa mkanda mzima, alishangaa na kuuliza: “Nyie nani kawaletea hizo habari, jamani watu wambeya sa...

Maneno ya kwanza ya Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle

Image
Jioni hii kwa hapa Tanzania habari zilianza kutoka kwamba Rafael Benitez amewasili St James Park kwa ajili ya kumalizia mambo ya mwisho mwisho. Guus Hiddink alisema kwamba Rafa Benitez ataleta uzoefu wa mkubwa kwa club ya Newcastle kama akiwa manager mpya wa club hiyo. Hatimaye Benitez amekua kocha mpya wa Newcastle united baada ya McClaren kufukuzwa kazi baada ya kikosi chake kuipeleka timu kwenye bonde la kushuka daraja. Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle alisema, “Nina furaha kuthibitisha kwamba nimefanya maamuzi na club kubwa ya England ambayo ina changamoto kubwa kwa sehemu ya ligi iliyobaki. Haitakua changamoto kubwa kwangu bali itakua kwa kwa wachezaji wangu,viongozi na mashabiki pia. Wote inabidi tuwe na lengo moja kwenye vichwa vyetu na nitaomba ushirikiano wenu kwenye hili.Mimi binafsi kurudi kwenye EPL ni kama kurudi kwenye familia yangu. Nahitaji ushiriki wenu kwa kikamilifu.”

Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA.

Image
Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA. Siku ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa  wanawake.   Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945,ilipofika tarehe 8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee.   Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali z...

Uzimaji wa simu feki na Dhana ya kupanga ni kuchagua -2

Image
Uzimaji wa simu feki na Dhana ya kupanga ni kuchagua -2 Wiki iliyopita msomaji wetu aliamua kupasuaji jipu kuhusu mada ya uzimaji simu feki, mawazo yake tumeyaheshimu na leo anaendelea kutoa hoja yake, fuatana naye: Ikumbukwe pia kuwa idadi kuwa ya Watanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi imeongezeka miaka ya karibuni kwa sababu ya kupatikana kwa urahisi na bei nafuu kwa simu na vifaa vyake. Ikiwa simu hizi zitazuiwa kwa kigezo cha kutokuwa halisi kwa sababu yoyote itakayotolewa na taasisi yetu ya umma (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania), Watanzania wengi wanaotumia simu hizi watakosa huduma hii. Wengi ni watu maskini wasio na uwezo wa kununua simu orijino za bei mbaya. Kwao hii ni anasa kubwa mno ambayo labda wapanga sera hawaioni kwa sababu kwao milioni ni fedha ndogo. Najua watakuja na hoja nyingi za kuhalalisha kuzima simu hizi feki baada ya hapa, ila tuangalie na mambo haya ya msingi. Tanzania inajiandaa kisera na kiutendaji kwenda kwenye nchi ya uchum...