RC Paul Makonda Amtembelea Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Ili Kupata Baraka Zake
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea
wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao ambapo jana
alimtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa ajili ya kupata baraka na
busara zake
Siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam.
Mkuu
huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili
afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo
kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya
kisasa.
Akizungumza
jana, alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuchukua busara
kutoka kwa wazee ili zimsaidie katika utendaji wake.
“Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Kwa
mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, leo anatarajia kukutana na Mufti Mkuu wa
Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Alhad Mussa Salum.
Comments
Post a Comment