Mauaji ya watu kinyume cha sheria, vurugu za makundi zaongezeka nchini Tanzania
Ugaidi
Polisi wa Kenya wa kutuliza ghasia wakipiga doria nje ya msikiti wa Masjid huko Mombasa, tarehe 31 Agosti, 2012. Ghasia ziliibuka katika mji wa bandari baada ya kuuawa kwa ulama mwenye msimamo mkali Aboud Rogo Mohammed. [Simon Maina/AFP]
Kenya kuongeza tahadhari kwa ajili ya njama za ugaidi wa al-Shabaab
Usalama
Wakulima kutoka mkoa wa Shabelle ya Chini wa Somalia wanarejea katika kupanda mazao baada ya maeneo mengi kukombolewa kutoka kwa al-Shabaab. [Tony Karumba/AFP]
Wakulima wa Somali wafurahia uhuru kutokana na utozwaji wa pesa kwa nguvu wa ...
Makosa & Sheria
Mzigo huu mkubwa wa heroini ulikamatwa huko Nairobi tarehe 14 Februari, 2013. Madawa hayo yalinunuliwa kutoka Tanzania na yalikusudiwa kupelekwa Uingereza. [AFP Photo/Stringer]
Tanzania yachukua hatua kali dhidi ya biashara ya magendo ya dawa za kulevya
Mazingira
Watu wakibeba miti waliyoiangusha kwa ajili ya mkaa huko Hargeisa. Wilaya tano za Galgadud zimeungana pamoja kuwazuia wakaazi kutokata miti ovyo kwa ajili ya kutengeneza mkaa. [Na Simon Maina/AFP]
Galgadud yapambana na ukataji miti kwa kupiga marufuku uzalishaji wa mkaa
Mauaji ya watu kinyume cha sheria, vurugu za makundi zaongezeka nchini Tanzania
Na Deodatus Balile, Dar es Salaam
Agosti 12, 2013
13 Maoni
Chapisha
Baruapepe
Panga upya Punguza Ongeza
Mauaji ya watu yanayofanywa na mamlaka za serikali pasipo kufuata sheria pamoja na vurugu zinazohusiana na makundi na uchawi vimegharimu maisha ya mamia ya Watanzania katika kipindi cha kwanza cha 2013, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) jijini Dar es Salaam.
Josephine Slaa, mke wa mpiga kampeni dhidi ya rushwa na mgombea urais William Slaa, anasaidiwa kuingia katika gari la polisi baada ya kupigwa na polisi waliokuwa wakipambana na ghasia wakati wa maandamano ya chama cha upinzani tarehe 5 Januari, 2011. Ripoti mpya iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu imesema mapambano baina ya raia na vikosi vya usalama vya taifa yamesababisha raia 22 na maofisa polisi 8 kufariki dunia katika nusu ya kwanza ya 2013. [Stringer/AFP]
Josephine Slaa, mke wa mpiga kampeni dhidi ya rushwa na mgombea urais William Slaa, anasaidiwa kuingia katika gari la polisi baada ya kupigwa na polisi waliokuwa wakipambana na ghasia wakati wa maandamano ya chama cha upinzani tarehe 5 Januari, 2011. Ripoti mpya iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu imesema mapambano baina ya raia na vikosi vya usalama vya taifa yamesababisha raia 22 na maofisa polisi 8 kufariki dunia katika nusu ya kwanza ya 2013. [Stringer/AFP]
Makala zinazohusiana
Walinzi binafsi wa usalama Tanzania kupata mafunzo ya kipolisi
Waandishi wa habari wa Tanzania wasusia matukio ya polisi
Tanzania inachunguza shambulio la kanisa Arusha, wananchi wako ukingoni
Wanaharakati wa Tanzania wataka kuona hatua za serikali dhidi ya kifo cha mwandishi wa habari
Wakati baadhi ya viashirio vinaonyesha kuboreka kwa kiasi ikilinganishwa na miezi sita ya kwanza mwaka uliopita, matokeo ya jumla ya kituo hicho yameibua wasiwasi kwamba Watanzania wanajichukulia sheria mikononi na kupuuza sheria iliyopo.
Vurugu za vikundi zilisababisha mauaji ya watu 597 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko kutoka vifo 563 kati ya Januari na Juni 2012, LHRC ilisema katika taarifa yake ya nusu mwaka iliyotolewa tarehe 29 Julai. Watu wengi kadri ya 303 waliuawa katika vurugu zilizohusiana na uchawi katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya 2013, ikipungua kutoka 336 katika kipindi kama hicho cha mwaka uliopita.
Katika vurugu za kuua ambazo zilitokea kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu, polisi wa Tanzania, wanamgambo na vikosi vya jeshi waliwaua raia 22, ambapo raia waliwaua polisi wanane wakiwa kazini, LHRC iliripoti.
"Mwaka uliopita, watu 31 waliuawa katika mauaji yaliyofanywa na vyombo vya serikali pasipo kuzingatia sheria mwaka mzima" Mwansheria na mtafiti wa LHRC Pasience Mlowe aliiambia Sabahi. "Miezi sita ya mwaka huu, tayari watu 22 wameshauawa. Kiwango kinaidaiwa kuongezeka."
Ripoti hiyo ilionyesha ongezeko la mauaji kutokana na fikra za haki za makundi, ulinzi hafifu wa haki za raia,ukiukaji wa uhuru wa kukusanyika, na kukosa taarifa, ni miongoni mwa mambo mengi.
Mlowe alisema kwamba LHRC ilikusanya idadi kwa ajili ya ripoti yake kutoka polisi, wanaharakati wa haki za binadamu na vyanzo vingine rasmi. Hivi vinajumuisha ripoti za makamishina wa wilaya ambazo LHRC ilitumia kubainisha majina ya waathirika na kupata ukweli wa msingi kuhusu mauaji.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Watanzania wanapambana na polisi wakati wanapohisi kwamba haki zao zinakiukwa, jambo linalosababisha hali hiyo kuongezeka kwa haraka na kusababisha mauaji.
Kama mfano, ripoti ilinukuu mauaji ya tarehe 11 Januari ya maofisa wawili wa polisi kwa kupambana na ghasia za madereva wa pikipiki, zinazojulikana kama boda boda, katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma. Maofisa hao waliuawa katika ulipizaji kisasi kwa polisi kurusha mabomu ya machozi katika msongamano wa waandamanaji tarehe 9 Februari.
Kwa kuongezea, ripoti inasema, wahalifu wa siku zote hawawatambui maofisa wa polisi kama mawakala wa utekelezaji wa sheria na wanajibu kwa vurugu kubwa wanapokabiliwa. Kwa hiyo, kutumia udhibiti zaidi, maofisa wa polisi wanatumia nguvu za ziada wakati wa kukabiliana na umma, kwa mujibu wa ripoti.
Pia imetaja mapigano kati ya madereva wa boda boda na polisi katika mkoa wa Mtwara mwishoni mwa Januari ambayo yalisababisha vifo vya raia. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini, vurugu zilianza wakati madereva walipopinga kukamatwa kwa dereva mwenzao wa boda boda na kuingia mitaani kupinga.
"Hatua ya waendesha boda boda ilikuwa kufanya fujo, zikisababisha uharibifu mkubwa ambapo majengo ya umma,mali za CCM [Chama Cha Mapinduzi] na zile za viongozi wao zilichomwa moto," ripoti hiyo ilisema. "Katika kuchukua hatua, polisi walitumia nguvu kupita kupambana na wafanya fujo na kusababisha vifo vya watu tisa na 11 kujeruhiwa vibaya."
Suala la uchawi linazidi kuongezeka
Ripoti iligundua kwamba idadi ya vifo kuhusiana na uchawi inaendelea kuongezeka nchini Tanzania, hususani mkoani Shinyanga.
Pamoja na vifo 303 vinavyohusiana na uchawi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, tatizo linaongezeka kufikia viwango vya mwaka 2012, wakati watu 630 walipouawa. Waathirika waliuawa kutokana na tuhuma kutoka kwa wanajamii wenzao kwamba wamewaroga watu.
Sheria ya Uchawi Tanzania, ambayo inakataza kitendo hicho, inaueleza uchawi kama "ushirikina, urozi, kufanya uchawi, matumizi ya vifaa vya kichawi, tendo la kukusudia la nguvu zozote za kiini macho na kukusudia kumiliki maarifa yoyote ya kiini macho."
Ripoti inadhania kuwepo kwa uchawi katika mgongano wa maslahi ya kiuchumi kati ya familia zilizo jirani, hususani katika kanda ya ziwa.
"Watu wanarogana wenyewe kwa wenyewe ili kudhibitiutajiri wa familia [au ukoo]," ripoti ilisema. "[Pia] kiwango kikubwa cha wasiosoma na imani za kishirikina na kuwatumia waganga wa kienyeji [inachangia katika mauaji]."
Ripoti inasema ukosefu wa huduma za msingi za matibabu kunachochea mamlaka na imani ya watu kwa waganga wa kienyeji.
Mwanasheria na mjumbe wa timu ya utendaji ya LHRC Imelda Lulu Urrio alisema ukimya wa serikali katika masuala hayo ulikuwa unasaidia kuchochea imani za kishirikina na kuwahamasisha wakosaji kufanya mauaji haramu.
"Kama haitazuiliwa mapema, inaweza kuishia kusababisha mauaji ya watu wengi na kusababisha mauaji ya kimbari," aliiambia Sabahi.
Mwanasheria Harold Sungusiya, ambaye anaongoza programu ya utetezi na mabadiliko ya LHRC, alisema serikali inapaswa kushughulikia uchawi na mauaji yanayohusiana na uchawi, vinginevyo itasababisha machafuko nchini.
"Mtu yeyote anayechukua sheria mkononi kwa kuwaua watu walioshutumiwa anavunja sheria," Sungusiya aliiambia Sabahi. "Ndiyo, wananchi wanaweza kuwa na imani ya msingi kwamba uchawi unafanyika lakini wanapaswa kuwa na imani katika mfumo wa sheria."
Sheikh Ali Mohamed Hemed, imam wa Msikiti wa Kisiwani huko Dar es Salaam, alisema viongozi wa dini wanapaswa kuwajibika kwa kiasi kikubwa katika kuuelimisha umma.
"Quran na Biblia zinawakataza kuwaua binadamu wenzenu," aliiambia Sabahi. "Tunapaswa kufanya zaidi kama watumishi wa dini kuwaongoa wafuasi zaidi kama njia ya kuistarabisha jamii yetu."
Mchungaji Kamala Simon wa Kanisa la Kilutheri huko Dar es Salaam alisema chanzo cha tatizo kilikuwa kuharibika kwa maadili.
"Tumepoteza mwelekeo wa imani, hivyo watu hawathamini maisha tena," alisema Simon. "Kama viongozi wa dini tunapaswa kufanya [jitihada] zaidi kuirejesha nchi tulikotoka. Tunastahili amani bila ya vurugu."
Watanzania lazima wazingatie sheria
Kikundi cha utetezi wa haki za binadamu kilipendekeza kwamba wananchi wafuate sheria na kuheshimu mamlaka yaliyotolewa kwa polisi kama wasimamizi wa sheria. Iliagizwa kwa mashirika ya kusimamia sheria kuheshimu haki za binadamu na kutumia nguvu zinazotakiwa pale zinapohitajika. LHRC pia waliomba serikali iingilie kati haraka kesi zinazohusu uchawi.
Mbunge Ismail Aden Rage aliiambia Sabahi mzizi wa vurugu ulikuwa ni ukosefu wa uelewa wa jinsi kila mwananchi anavyotimiza wajibu katika kulinda haki za binadamu na uhuru wa wananchi.
Kwa mfano wakati wa maandamano, ni wananchi gani wanaweza kufanya kwa haki, sheria za kushiriki zinapaswa kufuatwa ili kuhakikisha usalama wa vyama vyote, alisema.
"Watu wetu sasa wanaandamana dhidi ya hospitali, Benki Kuu na wakati mwingine ikulu," alisema Rage. "Viongozi wetu wa kisiasa wana wajibu wa kuwaelimisha wanachama wao [kutoyakabili] mashirika yetu ya kusimamia sheria."
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi alisema serikali imepokea ripoti ya LHRC na kwamba baada ya upitiaji wa kina itatoa mpango wa utekelezaji kuhakikisha kwamba sheria na haki za wananchi zimezingatiwa na kulindwa.
"Kitu cha msingi ni utawala wa sheria," Nchimbi aliiambia Sabahi. "Watu wote wanapaswa kufuata sheria ya nchi, na hakutakuwa na mauaji kama hayo. Kama serikali tutahakikisha kwamba hili linatekelezwa."
Comments
Post a Comment