Mohamud akutana na balozi wa Marekani kwa Somalia

Mohamud akutana na balozi wa Marekani kwa Somalia Agosti 27, 2013 + Toa maoni sasa Chapisha Baruapepe Panga upya Punguza Ongeza Rais Hassan Sheikh Mohamud alijadiliana uhusiano kati ya pande mbili na Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Somalia, James McAnulty, mjini Mogadishu siku ya Jumatatu (tarehe 26 Agposti), iliripoti Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa. Makala zinazohusiana Kuendelezwa kwa vikwazo vya silaha kwatishia mafanikio ya usalama nchini Somalia Kenya, Somalia na utata juu ya udhibiti wa Kismayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia Aadan: Somalia iko wazi kwa biashara Rais wa Somalia apongeza mipango ya Mpango Mpya Msemaji wa Rais, Abdirahman Omar Osman, alisema Mohamud na McAnulty pia walijadiliana mazungumzo yanayoendelea kati ya viongozi wa serikali ya shirikisho ya Somalia na wa mkoa wa Jubbaland mjini Addis Ababa, kongamano la kitaifa litakalofanyika baadaye mjini Mogadishu na hali ya usalama nchini humo. McAnulty aliahidi kwamba serikali ya Marekani itaisaidia Somalia. Vile vile siku ya Jumatatu, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia, Nicholas Kay , alipongeza maendeleo yaliyopatikana katika kuimarisha usalama katika hotuba yake kwenye mkutano wa Baraza la Usalama na Amani la Afrika, kiliripoti Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, Kay alisema kwamba jitihada za pamoja zilizoratibiwa kutoka serikali ya Somalia, nchi jirani na jumuiya ya kimataifa zinahitajika kufikia maendeleo ya maana. "Hatua inapigwa nchini Somala, lakini mafanikio yanaweza kurudi nyuma kama hatudumishi na kuongeza juhudi zetu za pamoja," alisema. "Kushindwa kufanya hivi kutakuwa na matokeo mabaya kwetu ndani na nje ya Somalia. Tusibahatishe kiasi hicho." Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2) (2) Like_icon Dislike_icon(0)

Comments

Popular posts from this blog

alahh hii ni kali ya mwaka madam Martha!-3