ARSENAL YAONGOZA ALAMA YA POINTI
Monday, December 9, 2013
ARSENAL YAONGOZA ALAMA YA POINTI
Klabu ya Arsenal imejinyakulia pointi moja baada ya kwenda sare ya bao moja dhidi ya Everton
Arsen Wenger aliwashirikisha wachezaji Jack Wilshere, Kieran Gibbs na Olivier Giroud baada ya kupumzishwa.
Gerard Deulofeu, iliipatia Everton nafasi ya kwenda sare na Arsenal huku ikiinyima Arsenal alama saba mbele ya mahasimu wake.
Deulofeu aliingiza bao hilo na kumaliza
matumaini ya Arsenal ya kupata alama nyingine tatu mbele ya mahasimu
wake licha ha Arsena kupata bao la Mesut Ozil.
Hata hivyo Arsenal inasalia kuwa mbele ya Liverpool kwa pointi tano.
Everton hata hivyo hawakuwa na wasiwasi wa mchezaji yeyote kuwa na jeraha.
Antolin Alcaraz alikuwa kwenye kikosi hicho lakini Leighton Baines, Arouna Kone na Darron Gibson walisalia nje.
Licha ya kuongoza orodha kwa pointi tano sasa,
baadhi wana shauku ikiwa kweli Arsenal inaweza kushinda kombe la ligi la
Premier,kwa sababu ushawishi wao kuweza kufanya hivyo bado haujawagusa
mashabiki wengi wa soka.
WANANCHI WA AFRIKA KUSINI WAENDELEA KUMUOMBEA MANDELA
Wananchi wa Afrika Kusini wanashirki maombi ya kitaifa ya mwendazake Nelson Mandela.
Siku hii ya maombi imesemekana kua siku ya kumkumbuka Mandela na maisha yake.
Rais Jacob Zuma atahudhuria maombi
hayo katika kanisa la Methodist mjini Johannesburg, wakishirikiana na
viongozi wengine kutoka dini mbali mbali kwa maombi yatakayofanyika siku
nzima leo.
Maombi maalum ya kitaifa yatafanyika siku ya Jumanne kabla ya kufanyika mazishi ya kitaifa Jumapili tarehe 15 Disemba.
Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikesha tangu Mandela kufariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Rais Jocob Zuma amewataka wananchi kwenda katika
viwanja vya michezo , makanisa, kumbi mbali mbali na sehemu zingine
zote za maombi, Leo Jumapili, kumkumbuka Mandela.
"Wakati huu tunapoomboleza kifo cha Mandela,
tunapaswa kuwa pia tunaimba kusherehekea maisha yake kwa juhudi za
mageuzi alizozifanya na kutuletea maisha mapya, tumuimbie Madiba,’’
alisema Rais Jacob Zuma.
Mrithi wa Mandela alipoondoka mamlakani, Thabo
Mbeki, atahudhuria maombi katika kanisa ya Oxford Shul synagogue mjini
Johannesburg mchana wa leo.
Viongozi wengine wakuu wa ANC, watahudhuria maombi katika maeneo mengine kote nchini humo,
KITUO CHA CHILDREN SUPPORT TANZANIA CHA ADHIMISHA SIKU YA ULEMAVU DUNIANI. MBEYA
Mgeni rasmi toka benki ya NMB akikata utepe kuzindua uwanja wa michezo wa kituo hicho |
Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupokea watoto tangu mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto zaidi ya 200. |
Mtoto Maxel mlemavu wa mikono na miguu nae akiwa katika vazi rasmi la mahafali ya kumaliza Darasa la awali kuingia darasa la kwanza |
SEREKALI YAOMBWA KUANZISHA BODI YA ZAO LA UFUTA
Serikali imeombwa kuanzisha bodi
ya zao la ufuta kama ilivyoanzisha bodi ya mazao ya pamba, kahawa na katani,
ili kuwawezesha kuwanyanyua kiuchumi wakulima wa zao la ufuta ambalo hivi sasa linalimwa
kwa wingi hapa nchini.
Imeelezwa kwamba bodi hiyo ya zao
la ufuta endapo itaanzishwa itawasaidia wakulima wake kunufaika kiuchumi, kwani
watakuwa na soko la uhakika kuliko hivi sasa wanapotapeliwa na walanguzi
wanaonunua zao hilo shambani mwao.
Ombi hilo lilitolewa na
baadhi ya wakulima wa zao la ufuta wa Tarafa ya Mbugwe, Wilaya ya Babati, katika
Mkoa wa Manyara, ambao walijengewa uwezo wa kulima zao hilo na shirika lisilo
la kiserikali la Farm Africa.
Mmoja kati ya wakulima hao
Theresia Njaiko mkazi wa kijiji cha Mwada, alisema endapo Serikali ingeanzisha
bodi ya zao la ufuta wakulima wengi nchini wangefaidika kwenye uuzaji kupitia
zao hilo linalolimwa kwa wingi nchini.
Mkulima mwingine wa ufuta Khadija
Juma mkazi wa kijiji cha Magugu, alisema japokuwa zao hilo halina bodi kama
mazao mengine ila wanategemea shirika la Farm Africa kwa kuwapatia elimu ya
kilimo hicho, mbegu, dawa na masoko.
Tabu Issa wa Magugu aliiomba
Serikali kutupia jicho kwenye zao hilo, kwani hivi sasa wakulima wengi
wamefaidika kupitia ufuta hivyo Serikari iwageukie na wao, japokuwa wanawezeshwa
na shirika hilo lisilo la kiserikali la Farm Africa.
Kwa upande wake, mkulima wa kijiji
cha Mwada Lucas Said alilishukuru shirika la Farm Africa kwa kuwawezesha
mafunzo, kuwapatia mbegu na kuwatafutia soko la ufuta, hivyo kuwasaidia
kuwanyanyua kiuchumi kupitia zao hilo.
Mkulima Juliana Agustino wa Mwada,
alitoa wito kwa Serikali iwasaidie wakulima wa ngazi ya chini, kuwawezesha
kushiriki maonyesho ya kilimo ya nane nane ili waonyeshe mazao yao na pia
kujifunza kupitia wakulima wengine.
Comments
Post a Comment