TAARIFA KWA UMA KUHUSIANA NA MKUTANO WA CHADEMA
TAARIFA KWA UMA KUHUSIANA NA MKUTANO WA CHADEMA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itafanya mkutano wake wa kawaida kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 20 hadi 21 Novemba, 2013.
Ajenda za mkutano ni kupokea, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu: Mihutasari ya mikutano iliyopita na yatokanayo na mikutano hiyo, taarifa ya hali ya siasa na ripoti ya fedha.
Ajenda nyingine ni pamoja na: taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba, taarifa ya utekelezaji wa Programu ya CHADEMA ni Msingi na shughuli za Kanda na taarifa ya utekelezaji wa Mpango Mkakati kuhusu maboresho.
Imesambazwa kutoka Uturuki tarehe 19 Novemba 2013 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
UWEPO WA WADHIBITI WENGI (REGULATORS) NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA NCHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la
Viwanda Nchini (CTI) Bi Christine Kilindu (Mwisho Kulia) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu hali ya viwanda nchini na mchango wa sekta
hiyo katika kupambana na tatizo la ajira katika kilele cha Siku ya
Viwanda Afrika, (Kati Kati) ni Kaimu Katibu Mkuu Odilo Otieno (Kushoto)
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda
(UNIDO) Emmanuel Kalenzi .
.Kesho ni kilele cha Siku ya Viwanda Afrika wananchi waombwa kujitokeza kwa wingi
.Tanzania yapiga hatua viwanda 700 vyaanzishwa ndani ya miaka mitano
.UNIDO yaifagilia serikali ya JK kwenye kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya viwanda
.Ujasiriamali kufundishwa kuanzia mashuleni
Na Damas Makangale, Moblog
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirikisho la
Viwanda Nchini (CTI) Bi Christine Kilindu amesema moja ya vikwazo katika
ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara ni uwepo wa wadhibiti wengi
(Regulators) na tozo ya ushuru wa asilimia 0.2 ni kizingiti kwa
maendeleo ya viwanda Tanzania. Moblog inaripoti.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya Viwanda Afrika ukumbi wa
Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, amesema moja ya mambo ambayo
yanawakwaza wawekezaji na wafanyabiashara ni uwepo wa wadhibiti wengi
katika sekta ya viwanda.
“Sisi hatujakataa kudhibitiwa ila
tulikwenda kumuona Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu na tulimweleza juu ya
matatizo ya kuwa na wadhibiti wengi na kila mtu ana taka asilimia zake
(percent) hiki ni kikwazo katika ukuaji wa sekta ya viwanda hapa
nchini,” amesema Bi Kilindu
Amesema kwamba pamoja na hayo lakini
kwa siku za hivi karibuni hali ya kutegemaa kwa nishati ya umeme
kumefanya sekta ya viwanda kupiga hatua kubwa kwani kwa sasa wanachangia
asilimia 10 ya ajira na asilimia 20 ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi.
Kilindu amesema shirikisho la viwanda
linaunga mkono kwa dhati kabisa dhana ya ujasiriamali katika kusukuma
gurudumu la maendeleo pamoja na kuanza kufundisha elimu ya ujasiriamali
mashuleni kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Viwanda toka Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Bi Elli Pallangyo
akizungumzia ukuaji wa viwanda kwa miaka ya hivi karibuni ambapo amesema
jumla ya viwanda 700 vimeanzishwa nchini.
“Tunataka elimu ya ujasiriamali katika
shule za msingi na sekondari ili vijana wetu waanze kufundishwa kuhusu
ujasiriamali na waondokane na dhana ya kuajiriwa na waweze kujiajiri,”
aliongeza
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi amesema katika
siku ya Viwanda Afrika ni muhimu kwa nchi na wadau wote wa maendeleo
duniani ksuhirikiana katika kukuza hali ya ujasiriamali miongoni mwa
jamii.
Amesema kuwa sekta ya viwanda ni
mhimili mkubwa katika kutokomeza tatizo la ajira kwa vijana kupambana na
umaskini na ni chachu ya ukuaji wa uchumi na pato la taifa.
Kalenzi alilisitiza kuwa shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda limejikita katika kufanya
utafiti na kuhamasisha uwekezaji wenye tija kwenye sekta ya viwanda
lakini viwanda vyenye kutoa ajira rasmi na inayoheshimika.
“Ongezeko la watu wasio kuwa na ajira
Afrika ni ushahidi tosha kwamba bara la Afrika linatakiwa kujikita zaidi
katika kuanzisha viwanda vipya na vinavyotoa ajira kwa sababu asilimia
63 ya watu walioajira Afrika wako katika ajira hatarishi,” amesema
Kalenzi
Kwa Upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Odilo Majengo amesema kwamba
viwanda vya uzalishaji ambavyo vipo nchini Tanzania vinaweza kuinua
uchumi wa taifa na kukuza pato la nchi.
“Kesho ni kilele cha siku ya viwanda
Afrika na ni muhimu kwa watanzania wote kushiriki katika maonyesho hayo
yanayoendelea katika viwanja vya saba saba ukumbi wa PTA kwani
wafanyabiashara wengi wataonyesha bidhaa zao,” amesema Majengo
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Masoko Odilo Majengo akisisitiza jambo katika siku ya
Viwanda Afrika ambayo kilele chake ni kesho hapa nchini. Kushoto ni
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda
(UNIDO) Emmanuel Kalenzi na Mwisho Kulia Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirikisho la Viwanda Nchini Bi Christine Kilindu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda toka Wizarani, Bi Elli Pallangyo
amesema kwa kipindi cha miaka mitano mpaka sasa taifa limeweza kupata
viwanda vipya 700 na pato la taifa kupitia vianda kufikia asilimia 9.
Bi
Pallangyo aliongeza sekta ya viwanda kwa miaka hivi karibuni imepiga
hatua kubwa za kimaendeleo na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa
na mauzo nje ya nchi.
Wakati
huo huo pamoja na serikali kutamba kwa uanzishwaji wa viwanda vipya
lakini Kuna baadhi ya viwanda vilivyokuwa vikifanya kazi miaka ya nyuma
hasa katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, lakini sasa havipo
tena baada ya watu waliokabidhiwa kushindwa kuviendeleza.
Baadhi
ya viwanda hivyo ni kama kiwanda cha nguo cha Urafiki Garments
kilichopo ubungo, Tanzania Dairies limited ambacho kilikuwa cha maziwa,
Ubungo Spining mill, pamoja na cha Zana za kilimo (UFI) ambacho kilikuwa
maalum kwa ajili ya kutengeneza zana za kilimo. Vingine ni Tanzania
Sewing Thread na Poly Sacks. Viwanda hivyo hivi sasa havifanyi kazi.
Viwanda
hivyo vilikuwa vinafanya kazi katika awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius
Nyerere, lakini sasa vimekufa kutokana na uzembe na kuridisha nyuma
sekta ya viwanda nchini.
Hivi
Karibuni, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda, alitoa
ripoti inayoonyesha jinsi hali ya viwanda ilivyo barani Afrika.
Ripoti hiyo ilijikita zaidi kwa nchi ya Tanzania ikionyesha jinsi viwanda vyake vilivyodorora.
Kigoda
anaelezea kwamba ripoti hiyo imejikita zaidi kutatua matatizo
mbalimbali ambayo yameikumba sekta ya viwanda.Anasema wanajipanga jinsi
ya kutatua matatizo yaliopo kwenye sekta hiyo ili kufufua viwanda na
kuleta maendeleo nchini.
Dk
Kigoda anasema Serkali itaweka mazingira bora kwa ajili ya kuvutia
wawekezaji, kuboresha na kulegeza masharti kwa wawekezaji, kuboresha
miundo mbinu, na kupambana pamoja na urasimu.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Emmanuel kalenzi akihojiwa na mwandishi wa MOblog.
“Ripoti
hii imejikita zaidi jinsi ya kutatua matatizo mbalimbali zinazoikumba
sekta ya viwanda nchini, naamini kwa kufanya hivi sekta ya viwanda
itainuka upya,” anasema Kigoda.
Dk Kigoda:Tufufue viwanda vyetu
Kutokana
na hali hiyo Serikali na sekta binafsi zinatakiwa kuungana ili kufufua
uchumi kupitia viwanda na siyo kutegemea kilimo tu kama uti wa mgongo wa
taifa.
“Mageuzi
ya fikra zetu yanahitajika kuitazama upya sekta ya viwanda na kuacha
kusema kwamba kilimo pekee ndio uti wa mgongo wa taifa letu kwani hata
nchi zilizoendelea zinathamini viwanda pia,” anasema Kigoda.
Waziri huyo anafafanua kwamba vitendo vinahitajika zaidi kufufua sekta ya viwanda.
“Lazima
tuondokane na nadharia na kujikita kwenye vitendo ili Wizara ya Viwanda
na biashara ipanue soko la ndani na nje, lakini hili litafanikiwa baada
serikali na sekta binafsi kuungana pamoja,”amesema Kigoda.
Anabainisha
kwamba tatizo kubwa linaloikumba sekta ya viwanda nchini ni ukosefu wa
mitaji na tatizo la kupatikana kwa soko la uhakika la kuuza bidhaa za
viwandani.
Anafafanua kwamba matatizo hayo yanasababisha kudorora kwa biashara katika nchi za Afrika.
“Ukosefu
wa mtaji kwa wafanyabiashara ni changamoto kuu inayowafanya washindwe
kuwekeza kwenye viwanda, hadi kufikia biashara katika nchi.
Kutokana
na kuwapo kwa tatizo hilo biashara imedorora kwa sababu imekuwa
ikifanyika kwa asilimia 10 tu ukulinganisha na nchi nyingine duniani.
Viwanda vinatumia mitambo duni
Katika
hatua nyingine wizara husika kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), imeandaa ripoti ambayo
imechambuliwa kiundani kuhusu maendeleo ya viwanda Tanzania ili
kuonyesha matatizo yanayokabili viwanda nchini.
Comments
Post a Comment