BIKRA SIO LAZIMA UTOKWE NA DAMU KWA TENDO LA KWANZA

BIKRA SIO LAZIMA UTOKWE NA DAMU KWA TENDO LA KWANZA

Bikira, mbona Damu haikutoka?
Habari dada dinah natumaini wewe ni mzima wa afya.
Nimekua nkifuatilia blog yako kwa ukaribu sana umekua ukitufundisha mambo mengi sana ambayo hata mie sikua nikiyafahamu hapo kabla. Pole sana kwa majukumu.

Mimi ninatatizo na nimeona wewe ni wapekee ambae unaweza kunisaidia tatizo langu, siku za karbuni nilipata mpenzi ambae aliniambia kua yeye ni bikra nilikubali kwa hilo.

Lakini siku ya siku nilifanya nae mapenzi ikiwa ni siku ya kwanza alilalamika sana anaumia ikabidi tuache, siku ya pili tukafanya tena kwa bahati nzuri uume wangu ulifanikiwa kuingia ndani vizuri na tukamaliza tendo kwa amani.

Lakini wasiwasi wangu naona kama amenidanganya coz marafiki zangu waliniambia kuwa unapofanya mapenzi na bikra lazima atoke damu kuashiria bikra yake imetoka.

Mpenzi wangu hajawahi kutoka damu sasa sielewi naona kama ananicheat, naomba unisaidie dada yangu kwani nilazima mwanamke bikra atokwe na damu katka tendo la ndoa ikiwa ndo mara yake ya kwanza?

**********

Dinah anasema: Namshukuru Mungu kwa uzima na afya njema. Ahsante kwa ushirikiano.

Umenikumbusha hadithi za magazetini enzi zile nipo shule....msimulizi anaandika "Nikamlaza, nikaanza mnyonya nini na nini kisha nikaingiza...Binti akalia sana kwa maumivu, nilipomaliza nikakuta shuka lote limelowa kwa damu"....


Hiyo ni fantancy, Bikira haloweshi shuka kwa damu unless katikati ya tendo Hedhi ikaanza, au wakati wa tendo Binti kuvunja ungo (inawatokea mabinti wadogo wanaolazimishwa kuolewa/bakwa) au umefanya kwa fujo sana mpaka ukamjeruhi mtoto wa watu au umembaka.

Enzi zile, Usiku wa Harusi/kutolewa Bikira Shangazi/Bibi/Kungwi anakuja na kijitambaa cheupe na kukipachika Ukeni ili kujua kama Bikira imetoka. Kwamba kukiwa na Damu shangwe, kikiwa kisafi Kilio....

Lakini kumbuka enzi zile Mabinti wengi waliolewa wakiwa wadogo na bila mapenzi so technically walikuwa wakibakwa na wengine kuvunjishwa Ungo kabla ya siku zao hivyo Damu ilikuwa ndio ushuhuda pekee!!

Pale ukeni (unapoingia uume/inapotoka damu ya Hedhi) huwa na kijiutandu ambacho kinaweza kutoka kutokana na shughuli za kimaisha au mtindo wa maisha.

Mf: Binti kufanya shughuli ngumu/za kutumia nguvu katika umri mdogo (kulima, kubeba maji, kupanda ngazi (watoto wa maghorofani mpo hehehehe).

Pia michezo, mfano Mpira, kuruka kamba, kuendesha Baiskeli n.k kunaondoa kile kijiutandu ambacho wengi ndio huesabu kuwa ni Bikira.


Ukweli ni kuwa, Bikira ni kutokufanya tendo la ngono (kutoingiliwa na mwanaume).

Nikijibu swali lako.... Hapana! Sio lazima damu imtoke mwanamke mara yake ya kwanza kufanya mapenzi.


Siku inayofuata baada ya tendo anaweza kuona uchafu uliochanganyikana na damu kwenye chupi ikiwa aliumia....inategemea ulimuingilia kwa nguvu kiasi gani.

Hali hiyo inaweza kuendela kwa siku mbili-tatu kisha akawa poa, again sio lazima kuwe na damu.
Mapendo tele kwako......: CHANZO: Dinahicious.blogspot.com
Share this article :
 

Comments

Popular posts from this blog

alahh hii ni kali ya mwaka madam Martha!-3