HATIMAYE MTANDAO WA MAWASILIANO TANZANIA VODACOM YACHANGIA MWENGE WA UHURU
Vodacom imechangia fedha hizo kupitia serikali ya mkoa wa Kagera ambao ndio wenyeji wa tukio hilo na kusema kuwa itatumia fedha hizo kulipia gharama mbalimbali ikiwemo za ukarabati wa uwanja wa Kaitaba pamoja mapambo katika uwanja huo uliotumika kwenye sherehe hizo kitaifa, matangazo na uhamasishaji.
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema kampuni yake wakati wote imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mambo mbalimbali ya kitaifa kwa kutambua umuhimu wa kufanya hivyo kwa masilahi ya taifa.
"Tumefanya kazi kubwa inayoonekana ya kusaidia maendeleo ya nchi yetu, sisi Vodacom tunatambua umuhimu wa kutoa mchango wetu kwa serikali na hata kwa jamii katika kile tunachoamini kuwa kwa kufanya hivyo tunatimiza wajibu wetu kwa jamii na taifa"Alisema Mwalim
"Tunachokifanya sasa hivi hapa Bukoba sio kigeni kwa Mkoa wa Kagera wala taifa kwani tuna mifano mingi ya kujivunia mkoani humu na sehemu nyengine mbalimbali za nchi ambazo Vodacom imechangia nguvu zake na kufanikisha matukio ya kitaifa na maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi."
Amesema mbali ya kuwafikishia huduma za simu za mkononi wananchi ikiwemo walio maeneo ya vijijini na kuwawezesha kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji mkubwa na wa gharama inaoufanya, Vodacom bado imekuwa ikitoa ushirikiano kwa serikali ngazi zote katika masuala ya maendeleo.
Mwalim amesema Vodacom itaendelea kutoa ushirikiano wake huo kwa serikali katika masuala mbalimbali huku akiushukuru Mkoa wa Kagera kwa kuipa nafasi Vodacom kwa kuiona kuwa inaweza kutoa mchango wake katika kufanikisha sherehe hizo za kitaifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe ameishukuru Kamouni ya Vodacom kwa mchango huo alioutaja kuwa ni mkubwa na uliosaidia sana kukamilisha maandalizi hasa uwanja wa tukio.
"tunawashukuru sana Vodacom kwa kukubali ombi letu la kusaidia jambo hili, mchango mlioutoa ni mkubwa sana"Alisema Massawe.
Amesema Vodacom inayokila sababu ya kupigiwa mfano kwani imekuwa na mchango mkubwa katika nchi hii ikiwemo kupitia huduma zake na michango yake kwa jamii.
Amesema Kagera ni mfano wa namna Vodacom ilivyofanya kazi nzuri ikiwemo kupeleka huduma za mawasiliano maeneo ya visiwani na yaliyo nje ya mji, ufadhili wa vyumba vya madarasa, matibabu kwa wanawake wanaopatwa na tatizo la fistula n.k.
Amesema wanachokifanya Vodacom minaenda sanjari na dhamira ya setikali katika kukuza ubia na sekta binafsi katika kushamirisha kasi ya maendeleo ya nchi na wananchi wake.
Akizungumzia Mwenge wa Uhuru, Massawe amesema ni moja ya tunu za taifa zenye lengo la kuimarisha na kukuza umoja,mshikamano na maendeleo ya taifa bila kujali imani za dini na itikadi za kisiasa.
Amesma mwenge huo mwaka huu mbali na kubeba ujumbe unaowahamasisha wananchi kushiriki katika kutoa maoni ya katiba, mkoani kagera utatumika pia kuangaza yale yote yanyoweza kuchangia kudumaza maendeleo,amani haki na mshikamano mkoani humo.
Comments
Post a Comment