JESHI LA ARDHINI LA ISRAELI LAINGIA GAZAKWA MSAKO MKALI KWA KUPITIA MAPIGANO YA ARDHINI


Sasa Israel yashambulia Gaza wakitumia vikosi vya angani, ardhini na majini
Israel imeanzisha operesheni ya nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya vuguvugu la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika ukanda wa Gaza.
Katika kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya wapalestina mia mbili wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Israel na Muisraeli mmoja aliuwawa katika mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka Gaza.
Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema lengo ni kuharibu kabisa miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na vuguvugu la Hamas kuishambulia Israel.
Vifaru karibu kumi vimeshuhudiwa vikielekezwa Gaza huku mashambulio ya angani na majini yakiendelea, ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema huenda hata hospitali zimegwa na mizinga.

Raia wa Gaza walia wakisema hamna pakutorokea huku mashambulizi ya Israel yakiongezeka
Watu zaidi ya 3 wamefariki katika duru hii ya mapigano mbali na wale zaidi ya 200 waliofariki awali.
Kundi la Hamas limesema watajibu oparesheni hiyo vilivyo lakini Israel inasema Hamas watapewa kipigo cha kudumu na kitakachowasambaratisha kabisa.
Israel imewaita maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kuweka nguvu zaidi katika operation hiyo.
Jana jamii ya kimataifa ilikuwa na matumaini makubwa kwamba huenda kukawa na usitishwaji mapigano wa kudumu baada pande zote mbili kukubali mapendekezo ya kusitisha mapigano kwa mda wa saa 5 za kuruhusu huduma za kibinadamu.
Mengi ya majumba na Miundo mbinu ya Gaza imebomolewa kwenye mashambulio hayo na maeneo mengi yanakosa hata maji safi ya kunywa.
Vilio na hali ya taharuki imetanda lakini pande zote mbili hazionekani kulegeza misimamo yao.
Huku Wapalestina wakikabiliwa na maisha hayo magumu katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan,wengi wa-Israeli waliokaribu na mpaka na Gaza wanaunga mkono operation hiyo, lakini wengine wanahoji gharama ya operation ya ardhini.

Comments

Popular posts from this blog

alahh hii ni kali ya mwaka madam Martha!-3