Juve yaponea tundu la Sindano kwa Inter – Penati zawabeba. Fainali sasa vs AC Milan
Juve yaponea tundu la Sindano kwa Inter – Penati zawabeba. Fainali sasa vs AC Milan
Aibu nusra iwakumbe wakubwa usiku wa kuamkia leo huko Italia ndani ya Jiji la Milan.
Mabingwa watetezi wa kombe la Coppa Italia Juventus leo wameepuka kuvuliwa ubingwa wao huo baada ya kukubali ushindi wao wa 3-0 katika mechi ya kwanza kule Turin kupinduliwa na vijana wa Roberto Mancini kwa kupigwa 3-0 na Milan ndani ya dakika 90 za mchezo marejeano. Lakini mwishowe bahati ikawa upande kwa kushinda kwa penati 5-3 na kutinga fainali.
Hata hivyo katika dakika 30 za nyongeza hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango ka mwenzake na hivyo mechi ikabidi iamuriwe kwa mikwaju ya penati ambayo Juventus wakaibuka na ushindi wa 5-4, beki wa kiargentina wa Milan Rodrigo Palacio akikosa penati na Leornardo Bonucci akafunga penati iliyoamua mechi upande aa Juventus.
Comments
Post a Comment