UCL: Madrid fainali ya 14, Atletico fainali 2 walizocheza zote ziliisha vibaya – hizi hapa takwimu 14 unazotakiwa kuzifahamu


Hatimaye michuano ya kombe la mabingwa wa ulaya inaelekea ukingoni kwa fainali itakayowakutanisha wababe wa jiji la Madrid – Real Madrid vs Atletico ndani ya Jiji la Milan.
 Kuelekea mchezo fainali tuanze kupata countdown ya matukio/takwimu yaliyotokea kuanzia kwenye hatua ya makundi mpaka nusu fainali kuelekea fainali.
1. Real Madrid wamefika kwenye fainali ya michuano ya ulaya/ChampionsLeague mara ya 14 sasa, mara nyingi zaidi ya timu yoyote.
2. Hii itakuwa mara ya 3 katika kipindi cha miaka minne ambapo fainali ya Champio League inachezwa na timu kutoka kwenye taifa moja.
3. Real Madrid wameshinda mechi zote 6 walizocheza katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wa Champions league – wakipata clean sheet mechi zote kwa maana ya kutoruhusu wavu wao kuguswa.
 4. Cristiano Ronaldo amecheza mechi ya 17 ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya – rekodi anayoshea na Xabi Alonso.
5. Sergio Aguero amefeli kufunga na kupiga hata shuti moja lilolenga goli katika mechi 5 za Champions League – ukame wake mkubwa zaidi katika Mashindano haya na Man City.
6. Keylor Navas amepata clean sheet katika mechi zake 12 za Champions League, sita kati ya hizo amepata Santiago Bernabeu.
7. Manchester City wametolewa kwenye michuano ya ulaya kwa mara ya 3 mfululizo na timu kutoka Hispania.
8. Kwa mara ya 3 mfululizo, kocha mgeni anafika fainali kwa mara ya kwanza katika msimu wake kwanza kwenye michuano. (Diego Simeone 2014, Luis Enrique 2015, Zinedine Zidane 2016).
9. Atletico Madrid wamefanikiwa kufuzu fainali wakati pia wakitimiza mechi 100 kwenye michuano hiyo.
10. Antoine Griezmann ndio mfungaji bora wa Atletico Madrid katika historia ya Champions League – akiwa na magoli 10.
11. Magoli 6 aliyofunga Xabi Alonso akiwa na Bayern ameyafunga nje ya eneo la penati.
12.Goli la Xabi Alonso ndio lilikuwa goli la kwanza Atletico kufungwa baada ya dakika 632 za Champions league.
13. Ni Cristiano Ronaldo pekee (magoli 10) ambaye amefunga magoli mengi zaidi katika hatua ya nusu fainali ya Champions League kuliko Robert Lewandowski (magoli 6).
14. Pep Guardiola ameondolewa kwenye michuano ya ulaya hatua ya nusu fainali kwa mara ya 4 mfululizo- mara 3 kati ya hiz ameondolewa na timu za Hispania.


Comments

Popular posts from this blog

alahh hii ni kali ya mwaka madam Martha!-3