Posts

Showing posts from March, 2016

Mange Kimambi Awalipua Wauza Unga Sakata la Mwanamuziki Chid Benz...Awataja Majina Laivu Bila Woga

Image
Kutokana na sakata la mwanahiphop Chidi Benz, Mwanadada Mange kawacha live wauza unga huku akiwataja majina baadhi ya makada maarufu wa CCM Kinje Ngombare na Iddy Azan kama wahusika wa hii game. Note: Magu anza na hawa waliotajwa maana kama Iddy Azan hii ni mara nyingine anatajwa... Ameandika hivi Kwenye ukurasa wake wa Instagram: From @mangekimambi_ - "Chi chi chi chi Chidi Benz... I respect huyu msanii sana. Ni Mtu wa kujitolea, about 4 years ago nilikuwa na event ya Watoto yatima pale Kurasini nikamuomba aje kuwafanyia show watoto, akaja kwa cost zake Na akafanya show bureeeeeeeeeeee. Sio wasanii wengi wanaokubali kufanya Hivi. So Leo nikimuona ana hali hii inanisikitisha mnoooo... . . Kweli binadamu tumeumbwa tofauti Jaman. I love money mpaka huwa naziota ndotoni Ila siwezi kufanya biashara ya unga au siwezi kuwa na mume muuza unga, yes ukiwa na mume muuza unga na wewe huna tofauti na mumeo Maana unakula hiyo pesa......... As much as I love mo...

Mkuu wa Wilaya Lucy Mayenga Aihofia Kasi ya Magufuli..Ajisalimisha na Kumuomba Rais Asimchague Tena Ukuu wa Wiliya

Image
Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote. Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti. Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zin...

Mashabiki Watafsiri Zari ana Mimba Baada ya Mdogo wake Diamond Kudaiwa Kuandika Ujumbe Huu

Image
Wakati Diamond yupo Ujerumani kwa ajili ya tour yake ya Ulaya, Jumatano hii katika mitandao ya kijamii hasahasa instagram kunasambaa ujumbe ambao mashabiki wengi wa Diamond wameutafsiri Zari ana mimba nyingine ya Diamond. Mtangazaji wa U heard ya XXL ya Clouds FM, Soudy Brown, alipost picha ya ujumbe huo na kuandika: Doh Blaza kishaloweka kwa Mara nyingine, haya T subiri mdogo wako on ze way. Sudy Baada ya ujumbe huo mashabiki wa Diamond amekuwa na maoni tofauti juu wa swala hilo. Nurashammy Safi sana Diamond waseme tena furaha mpaka nalala naviyato kwakwei kusikiya kama @zarithebosslady najuwa @diamondplatbumz haukosi kitu ila mimi kama shabiki wako ningependa kutowa zawadi ya tiffah Tajibetese Hivi nikweli naweza kufa kwa furaha @diamondplatnumz @zarithebosslady Nurashammy Safi sana @diamondplatnumz kusikiya kama @zarithebosslady ni mama kijacho ju yafuraha nalala na viyato kwakweli Mungu awape riziki Mchagga_wa_mashati Sijui na hii wata...

RC Paul Makonda Amtembelea Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Ili Kupata Baraka Zake

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao  ambapo jana alimtembelea  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  kwa  ajili  ya  kupata  baraka  na  busara  zake Siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam. Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya kisasa. Akizungumza jana, alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuchukua busara kutoka kwa wazee ili zimsaidie katika utendaji wake. “Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa ...

Zari wa Diamond Adaiwa Kumpa Makavu Laivu Kajala habari kamili ipo apo chini

Image
Kufuatia madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa na katabia ka’ kujiweka kimahaba kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa Sauzi, madai yametua mezani mwa gazeti hili kuwa, kimenuka kati ya Zari na Kajala. Chanzo chetu makini ambacho kimeomba jina lake lisitajwe gazetini kimedai kuwa, hivi karibuni baada ya Zari kupata ubuyu huo wa kuchovyewa penzi lake, alitafuta simu ya Kajala kisha kumpigia na kumpa makavu kuwa, asimuingilie kwenye himaya yake. “Siku moja nilikuwa na Kajala, mara ikaingia simu ambapo alipopokea akasikia sauti ya Zari, basi unaambiwa akamsema sana juu ya kuingilia penzi lake, Kajala akawa kimyaa, wala hajajibu lolote, inavyoonekana alipewa makavu,” alidai mtoa habari huyo. Baada ya kupata habari hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kajala ili kuzungumzia madai hayo ambapo alipokea simu na kupewa mkanda mzima, alishangaa na kuuliza: “Nyie nani kawaletea hizo habari, jamani watu wambeya sa...

Maneno ya kwanza ya Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle

Image
Jioni hii kwa hapa Tanzania habari zilianza kutoka kwamba Rafael Benitez amewasili St James Park kwa ajili ya kumalizia mambo ya mwisho mwisho. Guus Hiddink alisema kwamba Rafa Benitez ataleta uzoefu wa mkubwa kwa club ya Newcastle kama akiwa manager mpya wa club hiyo. Hatimaye Benitez amekua kocha mpya wa Newcastle united baada ya McClaren kufukuzwa kazi baada ya kikosi chake kuipeleka timu kwenye bonde la kushuka daraja. Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle alisema, “Nina furaha kuthibitisha kwamba nimefanya maamuzi na club kubwa ya England ambayo ina changamoto kubwa kwa sehemu ya ligi iliyobaki. Haitakua changamoto kubwa kwangu bali itakua kwa kwa wachezaji wangu,viongozi na mashabiki pia. Wote inabidi tuwe na lengo moja kwenye vichwa vyetu na nitaomba ushirikiano wenu kwenye hili.Mimi binafsi kurudi kwenye EPL ni kama kurudi kwenye familia yangu. Nahitaji ushiriki wenu kwa kikamilifu.”

Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA.

Image
Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA. Siku ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa  wanawake.   Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945,ilipofika tarehe 8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee.   Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali z...

Uzimaji wa simu feki na Dhana ya kupanga ni kuchagua -2

Image
Uzimaji wa simu feki na Dhana ya kupanga ni kuchagua -2 Wiki iliyopita msomaji wetu aliamua kupasuaji jipu kuhusu mada ya uzimaji simu feki, mawazo yake tumeyaheshimu na leo anaendelea kutoa hoja yake, fuatana naye: Ikumbukwe pia kuwa idadi kuwa ya Watanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi imeongezeka miaka ya karibuni kwa sababu ya kupatikana kwa urahisi na bei nafuu kwa simu na vifaa vyake. Ikiwa simu hizi zitazuiwa kwa kigezo cha kutokuwa halisi kwa sababu yoyote itakayotolewa na taasisi yetu ya umma (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania), Watanzania wengi wanaotumia simu hizi watakosa huduma hii. Wengi ni watu maskini wasio na uwezo wa kununua simu orijino za bei mbaya. Kwao hii ni anasa kubwa mno ambayo labda wapanga sera hawaioni kwa sababu kwao milioni ni fedha ndogo. Najua watakuja na hoja nyingi za kuhalalisha kuzima simu hizi feki baada ya hapa, ila tuangalie na mambo haya ya msingi. Tanzania inajiandaa kisera na kiutendaji kwenda kwenye nchi ya uchum...

Kigogo wa Serikali Amnasa Mkewe Gesti!

Image
Kigogo wa Serikali Amnasa Mkewe Gesti! Sakina Kisukari na njemba aliyekutwa naye gesti. Stori: Francis Godwin, UWAZI IRINGA: Mke wa kigogo mmoja wa serikali Mkoa wa Morogoro ambaye ni mwenyeji wa Wilaya ya Iringa, Kijiji cha Mlangali, Sakina Kisukari, amenaswa akiwa katika nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na mfanyabiashara ambaye inadaiwa ni mchepuko wake. Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la Mshindo, Iringa baada ya kufyatuka mtego uliowekwa na mume wa mwanamke huyo kwa kushirikiana na gazeti hili kabla ya kuwashirikisha polisi ili kuepusha damu kumwagika. Walivyokutwa gesti. Mtego huo uliwekwa kwa zaidi ya wiki mbili ili kufuatilia nyendo za mwanamke huyo ambaye aliondoka mkoani Morogoro anakoishi na familia yake kikazi na kuelekea Iringa kwa madai ya kwenda kuwasalimia ndugu zake. Hata hivyo, baada ya bosi huyo wa serikali (jina lake limehifadhiwa kwa h...

Mheshimiwa Zitto Kabwe Amuomba Rais Magufuli Atengue Agizo la Jakaya Kikwete

Image
Mheshimiwa Zitto Kabwe Amuomba Rais Magufuli Atengue Agizo la Jakaya Kikwete Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anatafuta nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli kumuomba atengue agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzuia ujenzi wa makazi katika Mlima wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji. Rais Kikwete alitoa agizo hilo mwaka 2006 kama moja ya hatua za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na kujaa mchanga kwa bandari ya Kigoma. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kigoma Cinema mjini Kigoma, Mbunge huyo alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuamini kwamba taarifa alizopewa Rais Kikwete zilizosababisha kutoa agizo hilo hazikuwa sahihi. Zitto alisema Rais Kikwete alipewa taarifa potofu kwamba mmomonyoko wa udongo kutoka katika eneo hilo ndiyo unaosababisha kujaza mchanga na kupunguza kina katika bandari ya Kigoma. Mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema kuwa tafiti zilizofanyika na taarifa zilizopo zinaonesha kuwa kup...

Dc -Paul Makonda Azindua Vitambulisho Vya Walimu Kupanda Daladala Bure Jijini Dar Es Salaam

Image

Mheshimiwa Waziri Mkuu wa tanzania amewatuma Mawaziri Watatu Kutatua Migogoro Ya Ardhi Simiyu

Image
Mheshimiwa Waziri Mkuu  wa tanzania amewatuma  Mawaziri Watatu Kutatua Migogoro Ya Ardhi Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atawatuma mawaziri watatu waje mkoa wa Simiyu ili wakae na uongozi wa kila wilaya pamoja na wananchi ili kubaini tatizo la mipaka baina ya wilaya hizo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana(Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa vijiji vya Mwakaluba na Mwandoya akiwa kwenye siku ya tano ya ziara yake mkoani Simiyu. “Tangu niingie hapa mkoani malalamiko ya mipaka nimeyapokea kila mahali nilikopita. Nimeamua kuwatuma mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi; Waziri wa Maliasili ua Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene waje mkoa huu kutatua matatizo yenu,” alisema. “…Nitawatuma waje na wapite kila wilaya, wakae na kuzungumza na wakuli...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 6

Image
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 6 ==

Mbowe Afunguka Sakata la Umeya Dar

Image
Mbowe Afunguka Sakata la Umeya Dar

Jamii Forums Wakimbilia Mahakamani....Wadai Kushinikizwa na Jeshi la Polisi Kutoa Siri za Wachangiaji wao

Image
Jamii Forums Wakimbilia Mahakamani....Wadai Kushinikizwa na Jeshi la Polisi Kutoa Siri za Wachangiaji wao Kampuni ya Jamii Media ambayo ni wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya Jamii Forums na FikraPevu, wamefungua kesi ya Katiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga amri waliyopewa na polisi ya kutoa taarifa binafsi za wanachama wao. Akizungumza baada ya kufungua kesi hiyo jana, Wakili wa Jamii Media, Shukuru Mkwafu alisema lengo lao ni kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwani vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Wakili Mkwafu alisema ili kulinda masilahi ya umma, lazima vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vizingatiwe. Alisema Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka 2015, inakiuka haki ya kikatiba namba 16 inayoruhusu kuwapo na hali ya faragha na kifungu namba 18 kinazungumzia uhuru wa kujieleza. Mmiliki wa tovuti...

Rais Magufuli Ampongeza Francis Cheka kwa Kutwaa ubingwa wa Mabara wa Uzito wa Super-Middle

Image
Rais Magufuli Ampongeza Francis Cheka kwa Kutwaa ubingwa wa Mabara wa Uzito wa Super-Middle Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amempongeza bondia Francis “SMG” Cheka kwa kutwaa ubingwa wa Mabara wa uzito wa Super-Middle wa chama cha WBF baada ya kumtwanga kwa pointi bondia Mserbia, Geard Ajetovic. Cheka alimchapa Ajetovic kwa ushindi wa majaji wote wa tatu katika pambano gumu lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club. Akitoa pongezi hizo jana, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa Rais amefuraishwa sana na ushindi wa Cheka ambao umeipa heshima nchi katika medani ya michezo ndani na nje ya mipaka yake.

Maalim Seif Arejea Zanzibar Akitokea India Kwenye Matibabu......Mamia ya Wafuasi wake Wampokea, Asema Polisi Imegeuka tawi la CCM

Image
Maalim Seif Arejea Zanzibar Akitokea India Kwenye Matibabu......Mamia ya Wafuasi wake Wampokea, Asema Polisi Imegeuka tawi la CCM Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana aliwasili Zanzibar kutoka ughaibuni na kulilaumu Jeshi la Polisi nchini akisema, “hapana shaka yoyote sasa limegeuka tawi la CCM.” Maalim Seif alisema hayo jana jioni wakati akizungumza na wafuasi wake waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume na baadaye kumsindikiza hadi nyumbani kwake Mbweni mjini hapa. Baadhi ya viongozi wa CUF waliohudhuria mapokezi hayo ni pamoja na Mansour Yussuf Himid, Nassor Ahmed Mazrui, Fatma Abdulhabibi Ferej na aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema chini ya mwavuliwa wa Ukawa katika urais wa Muungano, Juma Duni Haji. Maalim Seif aliyetokea India kupitia Falme za Kiarabu, alisema anaunga mkono kauli za Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wake, zilizosababisha ahojiwe na polisi juzi, kuwa “sasa CUF wamechoka na uhuni dhid...

Bomu Lalipuka Maskani ya CCM Zanzibar

Image
Bomu Lalipuka Maskani ya CCM Zanzibar Kitu kinachosadikika kuwa bomu kimeripuka usiku wa kuamkia jana eneo la Michenzani mjini Unguja, eneo linalojulikana kama maskani maarufu ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mlipuko huo umezua taharuki na hofu kwa wananchi wa eneo hilo hususan wanachama wa CCM ambao hukutana kwa wingi eneo hilo na kujadili masuala mbalimbali ya chama chao kuelekea uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu. Naibu Katibu Mku wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alilaani tukio hilo na kulielezea kuwa  liliandaliwa makusudi kwa lengo la kuwavunja moyo wanachama wa chama hicho. “Hili sio tukio la kwanza wala la pili katika eneo hili ambalo wanachama wetu walio msitari wa mbele wako wengi sana kwa kushirikiana na wanachama wengine.  "Hili ni tukio ambalo unaweza kusema limeandaliwa kwa makusudi na watu wenye dhamira ya kuwavunja moyo wanachama wetu na wapenzi wa CCM,” Vuai aliwaambia waandishi wa habari. ...

Ukiwa na tabia hizi,mwanaume lazima akukimbie!

Image
Ukiwa na tabia hizi,mwanaume lazima akukimbie! MUNGU ni mwema wapenzi wasomaji wa safu hii. Wikiendi nyingine tena tunakutana na kuweza kupeana darasa la uhusiano. Kujifunza ni muhimu, hakika ukifuatilia makala haya ya leo, utajifunza kitu. Twende pamoja! Kupitia safu hii nimekuwa nikipata malalamiko mengi kutoka kwa wanawake. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa. Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake. Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye kukimbiwa. Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama. Marafiki zangu, wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenz...

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Aamuru Kukamatwa Papo hapo Walimu 8 Kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Aamuru Kukamatwa Papo hapo Walimu 8 Kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi. Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013. Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel. Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga. Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajil...

Mkuu Wa Majeshi Aongoza Kuwaaga Maofisa Majenerali 16 Wa Jwtz Waliostaafu

Image
Mkuu Wa Majeshi Aongoza Kuwaaga Maofisa Majenerali 16 Wa Jwtz Waliostaafu MKUU wa Majeshi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange amewaongoza wanajeshi mbalimbali kuwaaga Majenerali 16 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambao wamemaliza muda wa utumishi wao. Sherehe hizo zilifanyika Uwanja wa Kambi ya Jeshi wa Twalipo, Mgulani jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana. Sherehe hizo ziliongozwa na bendi ya jeshi na gwaride maalumu. Miongoni mwa waliomaliza muda wao ni Meja Jenerali Samuel Ndomba ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na hadi anastaafu alikuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ. Wengine ni Luteni Jenerali Paul Mella ambaye alikuwa Kamanda wa Majeshi ya Kulinda Amani ya Darfur, Sudan na Brigedia Jenerali Harold Mziray ambaye alikuwa Mkuu wa Shule ya Infantria, Arusha. Majenerali wengine walioagwa ni Brigedia Jenerali Martin Mwankanye al...