Posts

Msani kutoka tanzania ambaye kwa sasa anayetamba na kibao chake nikumbushe Rayvanny afuata nyayo za Diamond

Image
Msanii wa muziki kutoka WCB Rayvanny, anaetamba na ngoma aliyoshirikishwa na msanii wa Kenya,Bahati, iitwayao “Nikumbushe” anazidi kufuata nyao za boss wake Diamond Platnumz. Rayvanny kutokea label hiyo ambayo kwa sasa inafanya poa kimuziki, ameonekana akipost picha zikimuonesha akifanya show katika studio za Coke zilizopo nchini Kenya. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa wasanii wa WCB kwenda kufanya show za ushirikiano na wasani wenzao kutokea bara hili katika studio za Coke. Rayvanny na GalaxiaEver Coke Studio Afrca hufanyika kila mwaka iliwa na lengo la kuwakutanisha wasanii wa muziki kutokea Afrika wanaofanya aina tofauti za muziki. Na Laila Sued

SMS NZURI ZA MAPENZI SOMA MTUMIE NA UMPENDAE

Image
Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo maana kila leo nayempata huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku waniaidi mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika? Nakupenda mpenzi. ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika japo mbinguni sijafika lakini nauhakika kwa kila mwanaume aliyeumbika na kukamilika akikuona lazima udenda utamtoka, naomba japo yako dakika nipate kukueleza moyoni yaliyonifika kwani siwezi tena kuficha jinsi navyokupenda, nakupenda amini kwako nimefika! ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ Nakupenda dear, amini moyoni umeniingia ndiyo maana mimba nikaamua kukubebea pasipo kunioa hakika mahaba yako yanifanya nijione malkia katika hii dunia! Nakupenda ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila kukicha usi...

“Eugena Washton” Mshindi Model Mpiga Picha Za Nusu Uchi {PLAYMATE OF THE YEAR} Wa Mwaka 2016,

Image
Model wa Marekani Eugena Washington ametajwa kua mshindi wa “Playmate of the year” kwa mwaka wa 2016. Playmate ni model ambae hupiga picha za nusu uchi nakuwekwa katika kurasa ya mbele ya gazeti la Playboy huko Marekani na mshindi hupewa kiasi cha $100,000 na gari.  Eugena amebahatika kushinda gari ambalo lina tarajia kutoka mwaka huu mwezi wa sita aina ya “124 Flat Spider”, na atakua ndo mmiliki wa kwanza wa aina hiyo ya gari. Eugena pia ni mshindi wa 57 tangu shidano hili lianze lakini pia ni mshindi wa tatu akiwa kama mwanamke mweusi kushinda katika shindano hilo la “Playmate”.

TUNDA LA WAREMBO DIAMOND,MAFIKIZORO WAUA UDOM,CHURA MPYA APATIKANA WAKIFANYA YAO NA BURUDANI .

Image
Msanii nguli wa bongo flavour  Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s”,a.a.a Simba pamoja na kundi la muziki la Mafikizolo wakiimba wimbo wao wa Color of Afrika wakati wa Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s” akiwaimbia kwa hisia wakati wa mashabiki wake waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana. Nyomi ya  mashabiki wa muziki waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Msanii wa muziki wa kundi la Mafikizolo kutoka Afrika ya kusini,Theo  Kgosinkwe  akionyesha umahiri wake wa kucheza muziki  katika Tamala la Vodacom kichuo zaidi lililofanyika  chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) jana

Kanumba kaondoka na filamu

Image
Kanumba kaondoka na filamu Marehemu Steven Kanumba  By Rhobi Chacha  ( email the author ) In Summary Hata hivyo kwa kuwa jambo hilo gumu na kwa vile kazi ya Mungu haina makosa, kwani yeyote anayemhitaji kwa wakati humchukua pasi na kujali nafasi yake katika jamii inayomzunguka. Kifo ni njia ya kila mmoja na limekuwa ni fumbo kubwa lisilo na majibu kamili.   in Share in Share ...

UCL: Madrid fainali ya 14, Atletico fainali 2 walizocheza zote ziliisha vibaya – hizi hapa takwimu 14 unazotakiwa kuzifahamu

Image
Hatimaye michuano ya kombe la mabingwa wa ulaya inaelekea ukingoni kwa fainali itakayowakutanisha wababe wa jiji la Madrid – Real Madrid vs Atletico ndani ya Jiji la Milan.  Kuelekea mchezo fainali tuanze kupata countdown ya matukio/takwimu yaliyotokea kuanzia kwenye hatua ya makundi mpaka nusu fainali kuelekea fainali. 1. Real Madrid wamefika kwenye fainali ya michuano ya ulaya/ChampionsLeague mara ya 14 sasa, mara nyingi zaidi ya timu yoyote. 2. Hii itakuwa mara ya 3 katika kipindi cha miaka minne ambapo fainali ya Champio League inachezwa na timu kutoka kwenye taifa moja. 3. Real Madrid wameshinda mechi zote 6 walizocheza katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wa Champions league – wakipata clean sheet mechi zote kwa maana ya kutoruhusu wavu wao kuguswa.  4. Cristiano Ronaldo amecheza mechi ya 17 ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya – rekodi anayoshea na Xabi Alonso. 5. Sergio Aguero amefeli kufunga na kupiga hata shuti moja lilolenga goli katik...

Mange Kimambi Awalipua Wauza Unga Sakata la Mwanamuziki Chid Benz...Awataja Majina Laivu Bila Woga

Image
Kutokana na sakata la mwanahiphop Chidi Benz, Mwanadada Mange kawacha live wauza unga huku akiwataja majina baadhi ya makada maarufu wa CCM Kinje Ngombare na Iddy Azan kama wahusika wa hii game. Note: Magu anza na hawa waliotajwa maana kama Iddy Azan hii ni mara nyingine anatajwa... Ameandika hivi Kwenye ukurasa wake wa Instagram: From @mangekimambi_ - "Chi chi chi chi Chidi Benz... I respect huyu msanii sana. Ni Mtu wa kujitolea, about 4 years ago nilikuwa na event ya Watoto yatima pale Kurasini nikamuomba aje kuwafanyia show watoto, akaja kwa cost zake Na akafanya show bureeeeeeeeeeee. Sio wasanii wengi wanaokubali kufanya Hivi. So Leo nikimuona ana hali hii inanisikitisha mnoooo... . . Kweli binadamu tumeumbwa tofauti Jaman. I love money mpaka huwa naziota ndotoni Ila siwezi kufanya biashara ya unga au siwezi kuwa na mume muuza unga, yes ukiwa na mume muuza unga na wewe huna tofauti na mumeo Maana unakula hiyo pesa......... As much as I love mo...

Mkuu wa Wilaya Lucy Mayenga Aihofia Kasi ya Magufuli..Ajisalimisha na Kumuomba Rais Asimchague Tena Ukuu wa Wiliya

Image
Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote. Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti. Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zin...

Mashabiki Watafsiri Zari ana Mimba Baada ya Mdogo wake Diamond Kudaiwa Kuandika Ujumbe Huu

Image
Wakati Diamond yupo Ujerumani kwa ajili ya tour yake ya Ulaya, Jumatano hii katika mitandao ya kijamii hasahasa instagram kunasambaa ujumbe ambao mashabiki wengi wa Diamond wameutafsiri Zari ana mimba nyingine ya Diamond. Mtangazaji wa U heard ya XXL ya Clouds FM, Soudy Brown, alipost picha ya ujumbe huo na kuandika: Doh Blaza kishaloweka kwa Mara nyingine, haya T subiri mdogo wako on ze way. Sudy Baada ya ujumbe huo mashabiki wa Diamond amekuwa na maoni tofauti juu wa swala hilo. Nurashammy Safi sana Diamond waseme tena furaha mpaka nalala naviyato kwakwei kusikiya kama @zarithebosslady najuwa @diamondplatbumz haukosi kitu ila mimi kama shabiki wako ningependa kutowa zawadi ya tiffah Tajibetese Hivi nikweli naweza kufa kwa furaha @diamondplatnumz @zarithebosslady Nurashammy Safi sana @diamondplatnumz kusikiya kama @zarithebosslady ni mama kijacho ju yafuraha nalala na viyato kwakweli Mungu awape riziki Mchagga_wa_mashati Sijui na hii wata...

RC Paul Makonda Amtembelea Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Ili Kupata Baraka Zake

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao  ambapo jana alimtembelea  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  kwa  ajili  ya  kupata  baraka  na  busara  zake Siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam. Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya kisasa. Akizungumza jana, alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuchukua busara kutoka kwa wazee ili zimsaidie katika utendaji wake. “Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa ...

Zari wa Diamond Adaiwa Kumpa Makavu Laivu Kajala habari kamili ipo apo chini

Image
Kufuatia madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa na katabia ka’ kujiweka kimahaba kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa Sauzi, madai yametua mezani mwa gazeti hili kuwa, kimenuka kati ya Zari na Kajala. Chanzo chetu makini ambacho kimeomba jina lake lisitajwe gazetini kimedai kuwa, hivi karibuni baada ya Zari kupata ubuyu huo wa kuchovyewa penzi lake, alitafuta simu ya Kajala kisha kumpigia na kumpa makavu kuwa, asimuingilie kwenye himaya yake. “Siku moja nilikuwa na Kajala, mara ikaingia simu ambapo alipopokea akasikia sauti ya Zari, basi unaambiwa akamsema sana juu ya kuingilia penzi lake, Kajala akawa kimyaa, wala hajajibu lolote, inavyoonekana alipewa makavu,” alidai mtoa habari huyo. Baada ya kupata habari hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kajala ili kuzungumzia madai hayo ambapo alipokea simu na kupewa mkanda mzima, alishangaa na kuuliza: “Nyie nani kawaletea hizo habari, jamani watu wambeya sa...

Maneno ya kwanza ya Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle

Image
Jioni hii kwa hapa Tanzania habari zilianza kutoka kwamba Rafael Benitez amewasili St James Park kwa ajili ya kumalizia mambo ya mwisho mwisho. Guus Hiddink alisema kwamba Rafa Benitez ataleta uzoefu wa mkubwa kwa club ya Newcastle kama akiwa manager mpya wa club hiyo. Hatimaye Benitez amekua kocha mpya wa Newcastle united baada ya McClaren kufukuzwa kazi baada ya kikosi chake kuipeleka timu kwenye bonde la kushuka daraja. Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Newcastle alisema, “Nina furaha kuthibitisha kwamba nimefanya maamuzi na club kubwa ya England ambayo ina changamoto kubwa kwa sehemu ya ligi iliyobaki. Haitakua changamoto kubwa kwangu bali itakua kwa kwa wachezaji wangu,viongozi na mashabiki pia. Wote inabidi tuwe na lengo moja kwenye vichwa vyetu na nitaomba ushirikiano wenu kwenye hili.Mimi binafsi kurudi kwenye EPL ni kama kurudi kwenye familia yangu. Nahitaji ushiriki wenu kwa kikamilifu.”

Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA.

Image
Siku ya wanawake Duniani na kauli mbiu ya CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA. Siku ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa  wanawake.   Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945,ilipofika tarehe 8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee.   Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali z...

Uzimaji wa simu feki na Dhana ya kupanga ni kuchagua -2

Image
Uzimaji wa simu feki na Dhana ya kupanga ni kuchagua -2 Wiki iliyopita msomaji wetu aliamua kupasuaji jipu kuhusu mada ya uzimaji simu feki, mawazo yake tumeyaheshimu na leo anaendelea kutoa hoja yake, fuatana naye: Ikumbukwe pia kuwa idadi kuwa ya Watanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi imeongezeka miaka ya karibuni kwa sababu ya kupatikana kwa urahisi na bei nafuu kwa simu na vifaa vyake. Ikiwa simu hizi zitazuiwa kwa kigezo cha kutokuwa halisi kwa sababu yoyote itakayotolewa na taasisi yetu ya umma (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania), Watanzania wengi wanaotumia simu hizi watakosa huduma hii. Wengi ni watu maskini wasio na uwezo wa kununua simu orijino za bei mbaya. Kwao hii ni anasa kubwa mno ambayo labda wapanga sera hawaioni kwa sababu kwao milioni ni fedha ndogo. Najua watakuja na hoja nyingi za kuhalalisha kuzima simu hizi feki baada ya hapa, ila tuangalie na mambo haya ya msingi. Tanzania inajiandaa kisera na kiutendaji kwenda kwenye nchi ya uchum...

Kigogo wa Serikali Amnasa Mkewe Gesti!

Image
Kigogo wa Serikali Amnasa Mkewe Gesti! Sakina Kisukari na njemba aliyekutwa naye gesti. Stori: Francis Godwin, UWAZI IRINGA: Mke wa kigogo mmoja wa serikali Mkoa wa Morogoro ambaye ni mwenyeji wa Wilaya ya Iringa, Kijiji cha Mlangali, Sakina Kisukari, amenaswa akiwa katika nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na mfanyabiashara ambaye inadaiwa ni mchepuko wake. Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la Mshindo, Iringa baada ya kufyatuka mtego uliowekwa na mume wa mwanamke huyo kwa kushirikiana na gazeti hili kabla ya kuwashirikisha polisi ili kuepusha damu kumwagika. Walivyokutwa gesti. Mtego huo uliwekwa kwa zaidi ya wiki mbili ili kufuatilia nyendo za mwanamke huyo ambaye aliondoka mkoani Morogoro anakoishi na familia yake kikazi na kuelekea Iringa kwa madai ya kwenda kuwasalimia ndugu zake. Hata hivyo, baada ya bosi huyo wa serikali (jina lake limehifadhiwa kwa h...

Mheshimiwa Zitto Kabwe Amuomba Rais Magufuli Atengue Agizo la Jakaya Kikwete

Image
Mheshimiwa Zitto Kabwe Amuomba Rais Magufuli Atengue Agizo la Jakaya Kikwete Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anatafuta nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli kumuomba atengue agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzuia ujenzi wa makazi katika Mlima wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji. Rais Kikwete alitoa agizo hilo mwaka 2006 kama moja ya hatua za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na kujaa mchanga kwa bandari ya Kigoma. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kigoma Cinema mjini Kigoma, Mbunge huyo alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuamini kwamba taarifa alizopewa Rais Kikwete zilizosababisha kutoa agizo hilo hazikuwa sahihi. Zitto alisema Rais Kikwete alipewa taarifa potofu kwamba mmomonyoko wa udongo kutoka katika eneo hilo ndiyo unaosababisha kujaza mchanga na kupunguza kina katika bandari ya Kigoma. Mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema kuwa tafiti zilizofanyika na taarifa zilizopo zinaonesha kuwa kup...

Dc -Paul Makonda Azindua Vitambulisho Vya Walimu Kupanda Daladala Bure Jijini Dar Es Salaam

Image

Mheshimiwa Waziri Mkuu wa tanzania amewatuma Mawaziri Watatu Kutatua Migogoro Ya Ardhi Simiyu

Image
Mheshimiwa Waziri Mkuu  wa tanzania amewatuma  Mawaziri Watatu Kutatua Migogoro Ya Ardhi Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atawatuma mawaziri watatu waje mkoa wa Simiyu ili wakae na uongozi wa kila wilaya pamoja na wananchi ili kubaini tatizo la mipaka baina ya wilaya hizo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana(Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa vijiji vya Mwakaluba na Mwandoya akiwa kwenye siku ya tano ya ziara yake mkoani Simiyu. “Tangu niingie hapa mkoani malalamiko ya mipaka nimeyapokea kila mahali nilikopita. Nimeamua kuwatuma mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi; Waziri wa Maliasili ua Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene waje mkoa huu kutatua matatizo yenu,” alisema. “…Nitawatuma waje na wapite kila wilaya, wakae na kuzungumza na wakuli...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 6

Image
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 6 ==